Mkopo nafuu kwa wafanyakazi

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Wakubwa,
naomba kueleweshwa ni Benki gani Tanzania inatoa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyakazi? Na riba hiyo ni kiasi gani? Asante.
 
kama upo DSM, DCB ni bank inayotoa mkopo wenye riba pungufu zaidi ya bank zingine, sisemi riba NAFUU kwani kilio cha wengi bado riba za mabenk zipo juu. DCB wanatoza riba ya 17% wakati bank zingine zinaizidi bank hii kwa 1-9%. Mbali na hiyo mashariti yao ya mikopo ni rahisi sana hayana mzunguuko sana kama sio ukiritimba.
 
Wakubwa,
naomba kueleweshwa ni Benki Tanzania gani inatoa mikopo yenye riba nafuu kwa wafanyakazi? Na riba hiyo ni kiasi gani? Asante.
Tanzania bara na visiwani kote kuna matawi ya Benki kubwa lakini Sikuambii mpaka useme unataka mkopo kwa shughuli gani....kwasababu nahisi ndiyo nyie mnaojaza foleni barabarani na magari ya mikopo...........lol
 
Mkuu nipe tu inshu. Kosa si la wanunua magari, ni la mfumo mzima unaoshindwa kudhibiti foreni na kuongeza matuta kila kukicha.
 
kama upo DSM, DCB ni bank inayotoa mkopo wenye riba pungufu zaidi ya bank zingine, sisemi riba NAFUU kwani kilio cha wengi bado riba za mabenk zipo juu. DCB wanatoza riba ya 17% wakati bank zingine zinaizidi bank hii kwa 1-9%. Mbali na hiyo mashariti yao ya mikopo ni rahisi sana hayana mzunguuko sana kama sio ukiritimba.

Nashukuru sana kwa ushauri huu, nimehangaika kupata mkopo Standard Chartered toka mwezi wa saba mpaka leo nazungushwa tuu kila siku naambiwa lete hiki, mara lete kile.
Nimelete
1. Barua ya mwajiri -Introduction letter
2. Confirmation letter,
3. Passport za ku mwaga
4. HR amesaini makaratasi kibao,
5. Company profile,
6. Barua ya Kitongoji
7. Specimen signature
8. Near location - identification

With all the above bado hawaja nipa hadi leo.
Nashinda pale kwao kila kukicha, yaani.
Napita kila section angalau nipate dokezo lakini wapi.
Kuna vijana wamekalia vitengo pale ukiwaangalia macho makavu naogopa hata kuwataja kwa majina
 
Tanzania bara na visiwani kote kuna matawi ya Benki kubwa lakini Sikuambii mpaka useme unataka mkopo kwa shughuli gani....kwasababu nahisi ndiyo nyie mnaojaza foleni barabarani na magari ya mikopo...........lol

Acha Mbwembwe. amesema "Mkopo nafuu kwa wafanyakazi" it is obvious this is consumption loan.
sasa unapotaka akuambie kwa sababu gani sikuelewei, alafu nilikuwa sijamaliza kukusoma, unaposema ndiyo nyie
mnaojaza foleni barabarani na magari ya mikopo ni kutaka kujipaisha tu. hauna lolote
 
Benki ya bakhressa unakopa sh 1 unarudisha sh 1 hawana riba wako kiimani zaidi
 
badala ya kumsaidia mnaanza majungu,badilikeni wana jf!!Mutensa,benki nafuu bila shaka ni nmb,riba yake kama sijakosea ni 16%,kwa visiwani nenda benki ya zanzibar,kama wewe ni mfanyakazi wa serikali wala hamna usumbufu wowote
 
mtu akileta mada toeni mchango wenye kujenga siyo kuwa kama watoto wadogo mtu kaleta mada ili apate msaada ajikwamu kimaisha na kama kukopa kwa kununua gari ni maamuzi yake
 
kwa dsm gari si anasa ni hitaji la lazima hasa kama unakaa nje ya mji au una mizunguko mingi, so unaweza pata hilo gari kwa mkopo au vyovyote, ushauri wangu kama umeajiliwa na umejiunga na mifuko ya jamii eg pspf nssf etc kopa huko riba zao ni 10% kwa mda wa miaka 2 hadi 5
 
Mmmhh mkuu una uhakika ni wao mifuko wanakopesha au ndio mpaka ujiunge kwenye saccos?
 
badala ya kumsaidia mnaanza majungu,badilikeni wana jf!!Mutensa,benki nafuu bila shaka ni nmb,riba yake kama sijakosea ni 16%,kwa visiwani nenda benki ya zanzibar,kama wewe ni mfanyakazi wa serikali wala hamna usumbufu wowote

Ulishawahi kupata mkopo katika taasisi hizo? tafadhali nijulishe utaratibu unaofuatwa!
 
Back
Top Bottom