Mimi sio mzoefu wa pombe yaani kichwa panzi.Basi kutokana na kuwa "bored" nikaamua kutoka na rafiki yangu kwenda bar ambaye na yeye sio mtumiaji sana wa vilevi.
Kufika bar tukakutana na jamaa ambao tunafahamiana,tukajiunga katika meza yao.Majamaa ni malevi kweli yakaanza konyagi ambayo zilikuwa mara yangu ya kwanza kuzinywa.
Kinachonisikitisha baada ya kuwa hoi kwa ulevi,ni matukio niliyoyafanya nyumbani kwa jamaa yangu.
1.Nilimtongoza msaidizi wake kwa kingereza ambacho hata hivyo kiuhalisia sikijui ananiheshimu sana.
2.Nilitapikia kitanda.
3.Mbaya zaidi nilikojolea TV chogo,kwa tetesi nilizopata imeharibika.
Sitaki tena pombe,nimeondoka asubuhi mapema bila wenyeji wangu kujua na hawajanitafuta,sijui rafiki yangu atanionaje nitaanzaje kuongea nae.Taarifa zote hizo kanipa mdogo wake sikumbuki chochote kuhusu tuhuma hizo.
Ushauri tafadhali.