MKE WANGU HAFANYI KAZI!
Maongezi kati ya mume na mwanasaikolojia.
Mwanasaikolojia: Unafanya kazi gani Bwana Mitomingi.
Mume: Nafanya kazi Benki ni Muhasibu.
Mwanasaikolojia: Mke wako anafanya kazi gani?
Mume: Hafanyi kazi, ni mama wa nyumbani tu naweza kusema ni goli kipa.
Mwanasaikolojia: Nani anaanda kifungua kinywa asubuhi?
Mume: Anaandaa mke wangu kwa kuwa hafanyi kazi.
Mwanasaikolojia: Ni muda gani mke wako huamka kuandaa kifungua kinywa?
Mume: Hua anadamka mida ya saa kumi na moja, kwa sababu hutakiwa kusafisha nyumba kabla ya kutengeneza kifungua kinywa.
Mwanasaikolojia: Watoto wako huwa wanaendaje shule?
Mume: Mke wangu huwapeleka kwa kuwa Hana kazi ya kufanya.
Mwanasaikolojia: Baada ya kuwapeleka watoto shule, mke wako hufanya nini?
Mume: Huenda sokoni, baada ya hapo hurudi nyumbani kwa ajili ya kupika na kufua nguo si unajua hafanyi kazi.
Mwanasaikolojia: Jioni baada ya wewe kurudi nyumbani kutoka ofisini, hua unafanya nini?
Mume: Napumzika baada ya kuchoka na kazi za ofisini za siku nzima.
Mwanasaikolojia: Mke wako hufanya nini muda huo wakati wewe umepumzika?
Mume: Huandaa chakula cha usiku, huawaogesha watoto, huniandalia chakula mimi, huosha vyombo, na kisha huwapeleka watoto chumbani kwao kulala.
***************
Katika hii story unafikiri nani anaefanya kazi nyingi?
Ratiba ya mke huanza mapema asubuhi mpaka usiku mwingi na hii ndiyo inayoitwa "HAFANYI KAZI"
Kuwa mke wa nyumbani haihitaji kuwa na cheti, stashahada, shahada ya uzamivu au uzamili bali majukumu kuhakikisha ustawi wa familia ni muhimu zaidi.
Waheshimuni wake zenu wanaofanya majukumu ya nyumbani kwa uaminifu kwa sababu sadaka wanayotoa haihesabiki. Hii ni kumbukumbu kwetu kwamba lazima tuheshimu majukumu ya kila mmoja wetu na panapo uwezekano tukasaidiana.