Mke wangu simuelewi kwa miaka 10 ya ndoa, naomba msaada

huyo mshkaji wako ni msharo uh aro, mi sioni tatizo hapo zaidi ya huyo mshkaji mwenyewe.
 
yaani ndoa ya miaka kumi ndo ina mambo ya kitoto kama hayo? mnapotezea watu muda...mtakua lini nyie? dah
 


Mpe pole huyo rafikiyo,inaelekea bado hajajua jinsi ya kuishi na mkewe.

Jana nilikuwa nasikiliza radio sijui ni ipi ila walikuwa wanaongelea maisha ya mume na mke ndani ya ndoa
yule mchungaji alikuwa akielekeza yale maongezi haswa kwa wanaume
na kuwaambia kuwa,ninanukuu "mke wako ni mtoto wako, yakupasa umlee, umsikilize, umdekeze, umliwaze
ingawaje huyo mtoto atakuwa anakuudhi, anafanya mambo ya ajabu ajabu lakini ye anaona kawaida, atakuwa haelewi unachosema ingawa ye anaona anaelewa..hivyo basi wewe mwanaume unapoishi na huyo mkeo yani mtoto wako,yakupasa umtreat kama mtoto wako wa kumzaa na umchukulie kama mtoto..si mnayajua maudhi ya watoto lakini?".mwisho wa kunukuu

Basi nikirudi kwenye mada, na kwa huyo rafiki yako hapaswi kununa.we wamnunia mtoto ye anakuona we ndo wa ajabu tena anakuona chizi
anapaswa akae nae chini amueleze kinachomkera kwani akikuna mwenzake hatajua kinachomsibu.
 
Pole sana ndugu yangu kwa maswaiba yanayo kukuta

Ndoa kama taasisi ina changamoto nyingi sana, jipo moyo, na jitahidi kutafuta chanzo cha mfarakano, tatua tatizo kisha maisha yatasonga.

Kwa mfano, kuna wanandoa walipata kuwa na mfarakano uliotishia ndoa yao kuvunjika, kwani mwanamke alikuwa ni kiguu na njia nyumbani hatulii, mara atakwambia nakwenda kusuka nyele za kimasai, hiyo inamchukua jumamosi na jumapili kuanzia asubuhi mpaka jioni, mara anaaga kwenda kwenye 'kitchen party' mara kwa shoga yake mtaa wa pili kunashuguli...... mume na mke kila siku ugomvi... na mara nyingi mke akitoka kwenye matembezi anakuwa amechoka na ikawa mara nyingi anageukia upande wa pili wa kitanda au anaangalia tamthilia kuvizia mume alale asiumbe tunda.

Huyu bwana uvumilivu ukamshinda, akatafuta ushauri kwa rafiki yake wa karibu, kabla ajachukua maamizi ya kuachana na mkwe, baada ya maongezi marefu, rafiki wa yule jamaa akamguzia kibao rafiki yake na kumueleza kuwa yeye ndio mwenye matatizo, alimpa ushauri kuwa siku amboyo mkewe atamuaga anataka kwenda matembezi ajitahidi kumpa mkewe mahaba ya kikweli kweli, [kwa kifupi jamaa alipewa desa ya jinsi ya kumtosheleza mkewe kimahaba]

Siku ya siku ikafika, ijumaa jioni wakekaa sebuleni, mke akamtaarifu mume kuwa anampango wa kwenda saloon kusuka nywele, jamaa alifurahi, na kuahidi kumuachia ufunguao wa gari na kisha jamaa akavuta wallet na kumkabidhi wekundu wa msimbazi watano, mke akaduwaa, wakiwa kitandani jamaa akakumbukia desa lake na taratibu akaanza kupractice, ndani ya saa 1 mke alikuwa hoi kwa mahaba aliyopewa.

Jumamosi ikafika, jamaa akaaga subuhi, akaondoka na kumuacha mkewe akiwa bado nyumbani, ilipofika mida ya mchana, mume akampigia simu mkewe kutaka kujua anaendeleaje na ususi, mke alisema bado yuko nyumbani anafanya usafi, jamaa aliporudi nyumbani jioni anakuta mkewe hajatoka yuko busy na shughuli za nyumbani, na maandalizi ya chakula cha familia, safari ya salooni ikafa.

Mume akaendelea kutumia shule aliyopewa, kwa uadilifu, kadri siku zilizidi kwenda mke akarudisha heshama na safari za mara kwa mara zikakoma.

Kwa kiasi kikubwa ufanisi mdogo wa mume mara nyingi ndio inakuwa chanzo kikubwa cha migogoro ndani ya nyumba

mwambia jamaa ani pm anipe story kikamilifu tuweze kusaidiana
 
Kwa kweli hutakiwi kununa bali kuongea na mkeo na atakuelewa, miaka kumi unataka kugombana na mkeo kwa ugomvi wa kipuuzi kiasi hiki, please acha kabisa ukisikia ya wenzako si ndio utaruka juu kabisa, Huyo mke ni mwerevu na ndio maana akiona unaanza malalamiko yako na gubu lisilokuwa na mbele wala nyuma anakupotezea na kujifanya anaangalia tv, kwa kifupi huyo mke ana akili sana mkuu you must be proud of her. Kuna wanawake wanajua sana misingi ya ndoa na hawana muda wa kupoteza kwa argument ambazo hazijengi. ACHA KUNUNA MWANAUME
 

Khaaaaaaaaaaaa!!!!!!! hii ni nzuri sana natamani wanaume wote wasome ili wafanye haya ya kwenye desa unayosema ni kweli kabisa, mke hatoki kwenye ndoa kirahisi, huwa tuko waoga sana mpaka yatufike shingoni .na mume akigeuka huwa tunarudi na kutulia tuliii, sababu hawa ndio tuliowapenda kiukweli toka moyoni ila wanatugeuka sana aiseee
 

Kama mke ni mtoto imagine mtoto ananuniwa na baba yake teheteheteheeeeetehe hata haikuji eee au unaonaje
 


Hiyo red hapo juu umenichekesha kwani kama alishawahi kumfumania inakuwaje??? teh teh
 

...Mwenye tatizo ni Mume.
Ajirekebishe mwenyewe kwanza.
Rudia tena kusoma hizo nyekundu.

...ajifunze yaliyopita yamepita, Mwambie
"katu hataweza yarudisha machozi machoni!"
 
huy jamaa f*l* kabisa vitu vidogo kama hivi anataka ushauri wa rafiki yake ? akikuta sms ya mapenzi kwenye simu ya wife si anaweza ua ?

Mkuu nina wasiwasi na mtoa mada. Itakuwa yeye ndo mhusika na anazuga. Hi sio jitu ya kuomba ushauri, tatua mwenyewe. Mbona watu wazima wanadeka sana?
 
Mume ur the problem, acha kununa mzee

...a.k.a "GUBU!"

Mkuu nina wasiwasi na mtoa mada. Itakuwa yeye ndo mhusika na anazuga. Hi sio jitu ya kuomba ushauri, tatua mwenyewe. Mbona watu wazima wanadeka sana?

...mnnnnhhhh!, ...taratibuni basi...
"midlife crisis" zinapochangia Usongo wa mawazo
-hupelekea wengi kushindwa kujitambua.
Kuomba msaada ruksa bana, LOL!
 
I don't pretend to know what love is for everyone, but I can tell you what it is for me; love is knowing all about someone, and still wanting to be with them more than any other person, love is trusting them enough to tell them everything about yourself, including the things you might be ashamed of, love is feeling comfortable and safe with someone, but still getting weak knees when they walk into a room and smile at you
 
utamaliza bucha nyama ni ile ile,wote tuna udhaifu cha msingi ni kutambua mwenzio anachukia nini na anapenda nini?je nawe ukikosea nikutafutie mume mwenzio?acha na mawazo finyu mpendwa.
 

Hata mimi hili naona ni kweli hujisahau mno baada ya kujitaabisha kupata mchumba
 
Nashukuru kwa ushauri wenu na tathmini yangu ya mjadala mzima inanionyesha Men ndiye mwenye matatizo na hii inawezekana ni kweli. Naomba mnipe muda nikamkalishe kikao tuongee kiutu uzima kama wanaume.

Wadau wa JF mbarikiwe saaaaana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…