Mke wangu ananitenga wakati wa kula pindi akitembelewa na dadaye

Sema Sasa

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
651
898
Siku zote kwenye familia yangu, mimi na mke wangu hula sahani moja milo yote inayoandaliwa kifamilia na wengine hujipakulia kwenye sahani zao.

Sasa kila akija dada yake, mimi baba hupakuliwa kwenye sahani yangu mwenyewe na mke wangu hujiandalia yeye na shemeji sahani moja.

Wadau nini tafsiri yake hapo na haki kweli kumwacha mumeo na kujilia na dadako. Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
 
Kawaida tu mkuu, usiumie. Unajua mtu ukitembelewa na ndugu yako mnakua na mengi ya kuongea...mmekumbukana....tena jinsia ya kike ndiyo kabisa...usichukulie vibaya
 
We tulia tu kama unanyolewa!"lazima kamati zikae"kuna shida gani akikutenga kula?kama angekunyima Chakula sawa.ungelalamika.
 
Anajua kuwa unakula kwa sauti kama dog hivyo ameamua kuwa anakupakulia sahani yako na kukuweka mbali naye yeye na dada yake ili dada yake asijue mapungufu katika ulaji.
 
Siku zote kwenye familia yangu, mimi na mke wangu hula sahani moja milo yote inayoandaliwa kifamilia na wengine hujipakulia kwenye sahani zao. Sasa kila akija dada yake, mimi baba hupakuliwa kwenye sahani yangu mwenyewe na mke wangu hujiandalia yeye na Shemeji sahani moja. Wadau nini tafsiri yake hapo na haki kweli kumwacha mmeo na kujilia na dadako. Ndoa na iheshimiwe na watu wote.
Ndoa yako ina umri gani ndugu yangu? Naona hujazungumzia watoto pengine bado ni ndoa changa. Najua mtakapokuwa na mtoto/watoto utatengwa zaidi.
 

"Ndoa na iheshimiwe na watu wote"

Aiseeeee hiii inamhushu dada mtu
 
Back
Top Bottom