Mke wa mtu sumu! Nusu nifumuliwe ubongo!

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,367
Reaction score
11,604
Imefikia hatua nimeona ni bora nirudi nyumbani Mwanza, nikae wiki kisha nirudi jijini Dar, jiji la biashara [emoji23][emoji23]

Katika pitapita zangu siku chache zilizopita, nilikutana na pic kali! Mzuri, mrembo n.k Kiukweli Mola anayakatakata maumbo! Nikam sound-isha, akaingia laini, tukaanza mahusuano!

Kesho yake nilimuita viwanja ili tuponde raha, lakini mtoto alikuwa na wasi wasi! Alikuwa akikaa anapapasa macho yake huku na huko, bia moja hakumaliza, alitoweka kurejea nyumbani! Nilipojaribu kumuuliza, alinambia kuwa yuko na mahusiano na hawala mmoja mwenye familia yake, anaishi Masaki! Mahusiano yao ni ya muda mrefu, amemzalia na mtoto, kwa sasa ana miaka minne! Nilitaka kuvunja mahusiano, lakini alisema itapendeza kama tukifanya kwa siri! Basi, roho ya mwanaume ni dhaifu, nikamkubaria!

Siku iliyofuata akanipigia simu, tukaenda mahali palipojificha kwenye ka grocery, tukapiga vizinga vya bia, akanipatia na pesa, laki tatu na nusu! Tukaagana, nikaamua kurejea nyumbani!

Cha ajabu nilipokuwa kwenye boda boda, niliona kama kuna bodaboda nyingine inanifuatilia nyuma hadi yule aliyenipakiza akaniuliza,"hivi hao walio nyuma yetu unafahamiana nao?" Nikamwambia hapana, akatumia kila aina ya technic zake zote alizojifunza huko VETA tukawapoteza!

Siku iliyofuata, tukaingia somewhere panafahamika sana! Wakati ananifanyia shopping nilishangaa kumuona mwanababa na kitambi chake anavuta mkono wa kuku (pistol), anakoki, nikaona isiwe tabu, ilikuwa full kukimbia ovyo, kilichoniokoa ni kwa vile nilikuwa kwenye watu wengi! Kama ingelikuwa sehemu ya wazi, hii ID ya man biznes ingeishia iyo siku!

Nilipofika mbali zaidi nikageuka nyuma, niliona wanaume wawili wenye miwani myeusi na suti wakinilia rada, nilikimbia kama chizi mpaka kituo cha daladala, nikaenda kulala kwa mshkaji, yeye ndio aliyeenda kunichukulia nguo kwangu! Asubuhi ya siku iliyofuta (juzi) nikapanda bus kuelekea huku home Mwanza! Pesa ya binti ikageuka kuwa nauli!


KARIBUNI MWANZA
Sema samaki ni wa kutosha! Nilikuwa nshawasahau Sangara! [emoji39][emoji39]
 
Sato bei juu!
 
Wangekutatua marinda ndiyo ungeujua utamu anaoupata huyo mgoni wako kwa huyo pic kali
 
Wewe umeshaolewa tayari, ukitua tu Dar wanapasua speakers
 
Reactions: EEX
Una bahati sana dogo, wale jamaa wenye miwani miyeusi waliokuwa wanakulia rada tulikuwa ni sisi. Leo wala usingeskia maumivu maana tulibeba LABRIKANTS
 
Wakati ananifanyia shopping nilishangaa kumuona mwanababa na kitambi chake anavuta mkono wa kuku (pistol), anakoki, nikaona isiwe tabu
hapa ndio ulipojichanganya na stori yako ionekane ya kupikwa, acha ujinga dogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…