Mke wa kutafutiwa vs Mke wa kutafuta mwenyewe

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Ningependa kusikia maoni juu ya hili,

Kwa upande wa wanaume kuna tofauti gani kati ya mke wa kutafutiwa yaani hapa ni kwamba wazazi wako au bibi na babu wanakuunganishia kwa msichana wanayemfahamu hasa kupitia wazazi wake na kukushauri umuuoe ingawaje wewe haumfahamu vizuri (msichana) au msichana unayekutana naye tu ulimwenguni na kuanza mambo ya sijui dating na mwishowe kuja kuamua kuona, kwenye hizo scenario mbili ipi unafikiri inamfanya msichana wako awe committed zaidi kwako?
 
Inatokana na akili yake ye mwenyewe anaweza akakaaa kinachotakiwa katika ndoa ni heshima na ustahamilivu wa hali ya juu tena sana ndo maana waswahili walisema ndoa ni ndoano walimaanisha hivi samak akikamatwa na ndoano kumtoa lazma umchane yaani umuharibu ni mara chache sana hutoka mzima so ndo kama ndoa mkija achana kazma mmoja wenu atakua na athar aiza mwanamke au mwanaume
 
Kinyago changu kitanifaa kama nikikichonga mwenyewe ....

Transcend (2016)
 
Mzazi akupeleke shule, akulishe, akuvalishe, akupe malazi bado unataka akutafutie mke? Uzazi huo siwezi. Samahani kwa kwenda nje ya mada.
 
Mzazi akupeleke shule, akulishe, akuvalishe, akupe malazi bado unataka akutafutie mke? Uzazi huo siwezi. Samahani kwa kwenda nje ya mada.
Mara nyingi wazazi wenyewe ndo uwa wanapenda kujibebesha huo mzigo
 
Tatizo ni kila kipindi na nyakati zake, imeonekana kuwa vjana wengi kwa sasa hawana mpango na slogan design hiyo!.
 
Mzazi akupeleke shule, akulishe, akuvalishe, akupe malazi bado unataka akutafutie mke? Uzazi huo siwezi. Samahani kwa kwenda nje ya mada.


Umesoma lkn nilichoandika na kuelewa au unajibu tu juu juu? Nimesema wazazi wenyewe ndiyo wanaamua kukuunganishia na wala siyo mtoto ndiyo anawaambia wazazi wamuunganishie!

Siku nyingine jaribu kuelewa kwanza ulichoulizwa kabla ya kukurupuka na kuanza kujibu siyo kwenye hii mada tu bali hata kwenye maisha yako itakuepusha na mengi!
 
Umesoma lkn nilichoandika na kuelewa au unajibu tu juu juu? Nimesema wazazi wenyewe ndiyo wanaamua kukuunganishia na wala siyo mtoto ndiyo anawaambia wazazi wamuunganishie!

Siku nyingine jaribu kuelewa kwanza ulichoulizwa kabla ya kukurupuka na kuanza kujibu siyo kwenye hii mada tu bali hata kwenye maisha yako itakuepusha na mengi!
Na wewe jaribu kumaliza sentensi nzima. Nimemalizia kwa kuomba msamaha cos nimeenda nje ya mada.
 
Tafuta mwenyewe, kuliko kila jambo likienda kombo urudi kwa wazazi kuwapa lawama
 
Kiukweli wa kutafutiwa huwa ni mke mwenye sifa za kua mke. Sio msanii, wazazi wanamjua vizuri na mke wa kutafutiwa huwa na faida zake nzuri.

Ila tatizo ni hisia zenu kuendana. Mara nyingi mnaweza msipendane kwa sababu kadha wa kadha.

Wa kujitafutia kwanza mnaendana. Kuna mutual feelings ila usanii mwingi.
Wengi wanaolalamikia wake zao hapo ninaamini (mawazo yangu) wengi walijitafutia.
 
Mara Nyingi Linapokuja Suala La Mke Kila Mtu Hua Na Vigezo Vyake Anavyo Vitaka. Hivyo Juu Ya Hili Inategemea Na Wewe Mwenyewe Unalichuliaje Jambo Hili. Maana Inawezekana Wewe Unampenda Mwanamke Mwembamba Ila Wazizi Wakakuletea Mnene. Hivi Je! Kunaweza Kuwa Na Upendo Wa Kweli Hapo?. Hivyo Bhana Kwa Kuondoa Lawama Zisizo Na Sababu Kwa Wazazi Wako Me Nakushauri Tu UTAFUTE MWENYEWE. Ili Hata Siku Ikitokea Mmemwagana Usije Kuwalaumu Wazazi Wako Kwa Kukuchagulia MKE Asie Faa.
 
Zirudi tu hizo zama za kutafutiwa mwanamke, haijalishi kuna commitment au vipi wanaume siku hizi midomo yenu imekua mizito utadhani mnakunywa uji wa magimbi.....ukiona mwanamke mdomo unasinyaa yani unakua kama "mimosa pudica"
 
Wazazi wetu wapendwa kwa kutangulia kwao kuliona jua kumewafanya wamejifunza mengi sana, baya na zuri na kwa kuyapitia hayo mengi wamekusanya busara nyingi sana....na wanajitahidi kwa hali kutumia hazina hizo za busara kutujenga na kutuweka mstari ulionyooka....

Wazazi wetu wanajua kuwa kumpata
mke au mume ni zaidi ya kuwa na sura nzuri, maumbile mazuri au kuwa na fedha nyingi benki.....

Wanatambua kuwa ndoa imara hudumishwa na UVMILIVU ndani ya ndoa...na ndio sababu wewe mpaka unafikia umri huo bado unawakuta wazazi wako wanaishi pamoja kwa furaha na heshima....

Vijana wengi wanakosea kwenye kupata wenza kwa kuwa vigezo wanavyodhani vinadumisha ndoa kumbe ndio vinaharibu ndoa...

Wanaingia kwenye ndoa wakiwa na fikra za kusadikika kuhusu utamu huku wakiziweka nyuma changamoto zake....

Kimsingi ni kwamba bado vijana wanaonyesha udhaifu mkubwa sana kwenye kuwapata wenza hivyo hawana budi kusaidiwa na watu wenye hekima na busara za hali ya juu kwani kuchagua mke sio sawa na kuchagua nazi gengeni....
 
Back
Top Bottom