Wanawake wengi wa sasahivi wamekuwa ni pasua kichwa katika familia zao.Wanafanya mambo ambayo yanachochea UGOMVI na chuki Kila mara.
ki katika hii dhambi pia.
Someni 1 Timotheo 2:12mpaka 13 .
Wanawake watapendeza ikiwa hawatakuwa watu wa kupayuka payuka na kuwapigia makele wanaume wao Bali itakuwa vyema na kupendeza ikiwa watakuwa watulivu na wenye heshima katika ndoa zao.Wawe na busara katika namna ya kuwaendea Waume zao yanapotokea matatizo wasiwapigie makelele Wala kuwapayukia au kuwa uchungu katika mioyo Yao Bali wayatatue wakiwa wapole na wanyenyekevu .
Ukweli ni kwamba wanaume ndio tumekua dhaifu ndio maana wanawake wanaonekana hivyo usemavyo. Sio kwamba wanawake hawataki kujitiisha kwa wanaume ila ni kwamba hawajisikii amani kujiachia mbele za wanaume, hasa wanaume dhaifu. Kiasili mwanamke ni mtiifu na anapokutana na mwanaume mtawala hujiachia kwake kwa sababu anajua yupo salama.
.
Wanawake wengi sikuizi wanaenda kwa waganga, au hata kubadilisha makanisa kila siku, kwa manabii ili wapate kujisikia ile hali ya kuwa chini ya kitu kinachompa changamoto. Kuna kitu wanakikosa kwa wanaume wa sasa, ambacho ni uongozi, kiurahisi anaenda kuupata uko japo kwa macho ya kawaida unaweza kuona kwamba wameenda kutafuta limbwata au kuomba kitu.
Mwanamke ambaye anaridhishwa na mwanaume wake kiroho, kiakili na kimwili ni vigumu kumkuta huko na hata akienda ni mara moja moja sana.
Ila tukisema wanawake ndo wachukue hatua na kubadilika, tutakua tunatwanga maji kwenye kinu sababu inajulikana mabadiliko yoyote yanaanza kwa kiongozi na kiongozi ni mwanaume, hivyo ni jukumu letu sisi kama wanaume kuchukua hatua na kuanza mabadiliko, wanawake watafuata tu na wote tutafurahia matokeo.
Mwanamke hataki kuchukua nafasi ya uongozi ya mwanaume ila sababu wanaume tumezubaa basi mwanamke ndio anajilazimisha kuuchukua uongozi ili jamii kiujumla isivurumuke kwa kukosa uongozi.
Vituko vingi wanavyofanya wanawake ni ishara tu kwamba kuna sehemu umelega na tukaze.
.
Cha kufanya sisi kama wanaume tuache kulaumu wanawake, tuanze kuchukua hatua. Tuchukue nafasi yetu ya uongozi. Maswala ya 50 50 kwamba na wenzetu nao inabidi wawe hivi tuyaache, tujiangalie sisi na kujiendeleza zaidi kuwa bora zaidi na kuwa viongozi.