Mke Mwenza

Mhhh very true wallahy,imepita io na imeeleweka na funzo nmepata kupitia iko kisa.
 
Ngoja niitafsiri na kuifupisha kwa lugha yetu tukufu kwa faida ya wengi.

Ni story ya mama mmoja.

Miaka kadhaa alikuwa kaolewa huyo mwanamke na waliishi maisha mazuri sana na mumewe wakiwa na watoto wa3, nyumba, duka na gari. Mumewe siku1 alikuja na kumwambia mkewe kuwa anampango wakuonheza mke wa pili. Mke alishtuka na kumwapia kuwa akimleta ataachana nae. Alimpenda sana mumewe na hakuwa tayari kushea na mwanamke mwingine. Pamoja na jitihada za mumewe kumweleza kuwa mwanamke anayetaka kumuoa ni single mother mwenye watoto wa4 ambae alitelekezwa na bwanaake na haijulikani alipo na anateseka sana, mke alikazia maamuzi yake kuwa katu katu hataki. Kama ana huruma sana, basi amsaidie pasipo kumuoa. Baadae mumewe alisitisha mpango wake na yakaishia hapo. Baadae yule mume alikuja kufa ghafla siku moja. Kila walichokuwa nacho kikasambaratika. Gari ikaishia, duka likafilisika na nyumba nayo ikatoweka. Umaskini ukamzidi, akaomba hifadhi kwa kakayake na akapokelewa ambapo aliishi kwa kusumangwa sana na wifi na kushindia makombo. Kakayake akamletea habari kuwa kuna mwanaume anahitaji mke wa pili na anampenda hivyo kama yupo tayari awaunganishe wakutane. Alikumbuka namna alivyopinga ukewenza alipokuwa na mumewe lakini safari hii alikuwa hana jinsi kwani alikuwa akiswali sana akimuomba Mungu ampe mume amsitiri. Hakuwa na ujuzi wowote hata wakufanya kazi hivyo alikuwa tayari pasipo hiyana. Kukutana na yule bwana, akaambiwa kuwa mke wa kwanza hajaafiki ila ataenda kumshawishi akubali kuongezewa mke mwenza. Yule mama alirudi nyumbani akisali sana na kumuomba Mungu yule mke wa kwanza akubali. Mkewakwanza alikubali ingawaje kwa shingo upande na walikutanishwa. Yule mke wa kwanza alimpa mkono huku akilia na kumwambia ingawaje ni vigumu sana ku share mume, nimekubali na kuridhia tuwe sister(wakewenza). Kisha aliolewa na kusitirika. Akakumbuka ni namna gani akikuwa na moyo mgumu kumruhusu mumewe kumsitiri yule mwanamke aliyekuwa na watoto wa4. Aliumia sana na kujifunza kitu maishani. Hujafa hujaumbika.
 
Hii lugha hapana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reactions: JMF
ASANTE SANA MKUU HIZI STORI WAWE WANAANGALIA LUGHA MIMI SIKUELEWA ATA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
A Very powerful story....may Allah makes it easy for our sisters in finding pious husbands
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…