Hapo kulikuwa na tatizo siku nyingi sema kaka yako hakuling'amua mapema, Mtoto wa mwaka mmoja unampeleka kwa mama , kwa kweli hiyo si hakikabisa ,huyo mama yake alikuwa na uwezo wa kumlea huyo mtoto hata kama angekuwa hana baba na akapata matunzo mazuri sana.
na ndiyo watoto wa siku hizi wamekuwa watukutu, hawana upendo, wakatili, vibaka, vurugu mtindo mmoja kwa sababu hawapati malezi yaliyo thabiti kutoka kwa mama zao.Unakuta mtu amezaa anamnyonyesha mtoto maziwa ya kopo, cerelac na mavyakula ya kizungu ili asinyonyeshe , na unakuta hana tatizo lolote anadai hataki kunuka maziwa, this is not fair kwa kweli.Halafu tunalalamika watoto wametushinda , wakati source ni sisi wenyewe kupeleka watoto wakalelewe na watu wengine , so wanakuwa na Tabia za ajabu ajabu.
Ushauri mwambie kaka yako akae atulie tuli, kwa Muda huu maana hana kazi.
Pili akishapata kazi ajipange atamleaje huyo mtoto maana hapo hamna ndoa tena.
Yale ambayo yamejificha leo atayaona moja baada ya lingine, lakini akikurupuka kufanya uamuzi hatoweza kubaini kinachomfanya mkewe kuwa na kiburi cha hivyo na kupelekea kufanya maamuzi yake peke yake.
WASWAHILI WANASEMA MWISHO WA UBAYA AIBU.