Mke apigwa faini kwa kufungua simu ya mumewe

BOB OS

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
3,431
6,848
130717163110_simu_tanzania_640x360_bbc.jpg


Mwanamke mmoja katika muungano wa milki za kiarabu amepigwa faini na kurudishwa kwao baada ya kupatikana akiingia katika faragha ya mumewe.

Vyombo vya habari vinasema kuwa mwanamke huyo alichukua na kufungua simu ya mumewe baada ya kumshuku kwamba alikuwa na uhusiano wa kando.

Mumewe alilalamika kwa maafisa wa polisi na mkewe akashtakiwa chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni, kulingana na chombo cha habari cha Gulf News.

Mwanamke huyo ambaye jina lake lilibanwa na ambaye ni mgeni katika muungano wa milki za kiarabu alipigwa faini ya pauni 28,000.

Alikiri mahakamani kwamba aliifungua simu ya mumewe bila ya ruhusa na kuzituma picha katika simu yake wakili wake aliiambia Gulf News.

Wakili huyo Eman Sabt,alisema kwamba wanandoa hao walikuwa na umri wa miaka ya 30 na wenye asili ya kiarabu,lakini hakutoa maelezo zaidi.
 
Hii sheria ikija huku bongo wanaume tutanenepa aiseee.

Yaani full kukaguliwa kaguliwa na wake zetu, mpaka kwenye soksi wananusa nusa, sijui wanatafutaga nini huko.

Najiulizaga hivi kale ka uvundo ka kwenye soksi hawakasikiagi.??
 
TZ ni bingwa na copy and paste kwa nn hawaoni haja ya kufanya hivyo kwenye sheria hii?
 
ukiona sijashika yako hata yangu huruhusiwi. mim ata ya mama / baba siishiki itaita wee wala simwambi km inaita mpaka aisikie mwenyewe.
 
ukiona sijashika yako hata yangu huruhusiwi. mim ata ya mama / baba siishiki itaita wee wala simwambi km inaita mpaka aisikie mwenyewe.
 
Back
Top Bottom