niliishi na mwanamke tukapata mtoto mmoja ikatokea cku moja nipo kazini kasomba vitu vyote katoroka siku hizi anabembeleza eti nimsamehe shoga yake ndo alimwambia atoroke karudi na mwanangu kwangu nikimfukuza ataondoka na mtoto anadai sitakuja kumpata huyo mtoto tena .kwa upande wa sheria bado anaharali ya kubaki na mtoto yaani mtt yk chini ya miaka saba naombeni ushauri nimtimue mtoto atakuja baadaye kunitafuta au nimsikilizie wakati namlea mtoto wangu? ushauri tafadha
Msamehe tu mradi kajua kosa lake na kajutia,sababu usipomsamehe utakuwa unamtesa mototo ambaye ni innocent,na bado ni MDOGO anahitaji mapenzi ya baba na mama,na isitoshe mtoto ana thamani kuliko vitu vilivyoibiwa na huenda mpaka sasa kuna vitu vingine ulishanunua kufidia,hivyo msamehe kwa faida ya mwanao!!!
Kumbuka watu wanavumilia mengi kwenye ndoa kwa SBB ya watoto!!watu wanasalitiwa lkn wanasamehe kwa faida ya watoto!cha msingi kama aliondoka kitambo hakikisha mnapima VVU!
Mwizi habadiliki hata afungwe miaka mia akifanikiwa kurudi anaendelea na kazi kwa sababu tayari amelaaniwa na kutwishwa zigo la wizi. Amerudi kuchukua tena ulivyonunua. Umenishangaza eti anakutisha na mtoto....Mwache amtunze kama nguvu zipo na akishindwa amrudishe.
hiyo kawaida mbona, we kama unampenda kubali yote, m namjua dada mmoja alkua anakaa na mwanaume bila kuoana wakagombana akasomba kila kitu ndani, badae akarud na mume kamuoa, na hawana hata motto, sembuse wew ulyezaa nae, mapenzi upofu babu eeh ukisema uangalie makosa yake hamtofika...
Nina tatizo kama lako kaka, ni kweli huyo mwanamke hafai kabisa tena ila kwa faida ya mtoto wenu, hakikisha mnapima vvu kwanza kisha msamehe na mumlee mwanenu, mie mpaka leo hajarudi nami najikaza kiume huku natafuta tu rafiki wa kike maana jambo hilo linanishughulisha sana kichwani mwangu na anasema hawezi kuja mpaka nimfuate kwao, nami siwezi kwenda kwao kwa 7bu sikumfukuza, akipenda atakuja na asipopenda..basi
Pole sana ndugu. Alipoondoka na mali zako na mtoto alifikiri kuwa mtoto kazaaje? Huyo mtoto ni wako tu hata aende naye wapi. Ukimkaribisha ndani tena unajiletea majanga. Shauri yako
pole sana kwa hlo.we kabla hamjafanya makubaliano kuwa arud nymbn inabdi umshawish mkapme kwanza huwezjua alpoondoka alfanya mambo gan huko nyuma alafu ukijua nimzma msamehe ulee mtoto wako