Mkapa aomba kazi yoyote kwa Magufuli

Big Mo

Member
Jul 28, 2015
96
19
POSTED THURSDAY, JANUARY 7, 2016 | BY- SAULI GILIARD, MWANANCHI DIGITAL

Mkapa: Niko tayari kufanya kazi yoyote nitakayopangiwa

Rais mstaafu Benjamin Mkapa amesema yuko tayari kufanya kazi yoyote na kutoa ushirikiano wake

Rais Dk John Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar leo. Picha na Ikulu

Dar es Salaam. Rais mstaafu Benjamin Mkapa amesema yuko tayari kufanya kazi yoyote na kutoa ushirikiano wake kwa serikali ya Rais John Magufuli endapo atahitajika.

Mkapa aliyeambatana na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba ametoa kauli hiyo leo punde baada ya kukutana na Rais John Magufuli Ikulu, Dar es Salaam.

“Rais Mstaafu Mkapa pia amemhakikishia Rais Magufuli kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano wakati wote ama kufanya kazi yoyote endapo atahitajika kufanya hivyo,” taarifa iliyotolewa na Ikulu leo mchana imeeleza.

Kwa mujibu wa Ikulu, malengo ya mkuu huyo wa zamani wa nchi kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na Watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, waziri mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba amempongeza katika juhudi zake katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na kuelekeza matumizi kwenye maeneo muhimu ambayo yanawahusu wananchi yakiwemo afya na maji.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Jaji Warioba amewataka Watanzania wote kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kazi anazofanya ikiwemo kukomesha rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na wizi wa mali ya umma.

"Lazima kila mmoja amuunge mkono Rais, tusije tukamuachia, pale ulipo kama ni mambo ya rushwa uanzie hapo hapo, kama ni mambo ya matumizi mabaya ya madaraka anzia hapohapo, tusije tukamuachia Rais pekee yake, yeye awe kiongozi wetu, lakini Watanzania .
 
Mkapa apewe wizara isiyo na ofisi maalumu, naamini yule mzee anamapenzi ya dhati na nchi hii.

Ila wanamtandao ndio waliomfanya awe fisadi kwa lazima
 
Last edited by a moderator:
Huyu si ameshastaafu au ndio Njaa imekuwa Kali Uraiani? Aachie na vijana wapate kazi sasa kama kazi zichukuliwe na Wazee huku vijana hawana Ajira.... Magufuli naomba umpuuze huyu Mzee... Alishakuwa Jirani yetu hana Ujamaa.... kabisa ndio anataka kuja kutukana tena Wananchi maana kaona tu Wapumbavu sasa anataka kuongoza tena.... Kila zama na zama zake mwambie Akawatumikie wana mtwara aliowatelekeza kaenda kuishi Lushoto na Masaki ya Dar...
 
Mzee aendelee tu kupumzika aki-enjoy pension isiyo na vikwazo...

Kazi aliyoifanya kwenye kampeni/uchaguzi inatosha sana na abaki tu kuwa "Mzee Mshauri"
 
Hana Lolote kipindi kile anajiuzia mgodi kwa 75m alikuwa hataki kuijenga Nchi?
 
Kwa mujibu wa Ikulu, malengo ya mkuu huyo wa zamani wa nchi kukutana na Rais Magufuli ni kumpongeza kwa dhamana aliyopewa na Watanzania kuiongoza nchi, kuunda serikali na kumtakia heri ya Mwaka Mpya.

Hivi angepiga simu, video conferencing au skyping, si angeokoa pesa za umma? Yaani alifunga safari ya kwenda kumpongeza? Taifa hili, kazi ipo.
 
Huyu aliyeuza NBC, Air Tanzania na vitu vingi tu. Hii ni aibu kubwa kuja na upuuzi kama huu. No way back na ndiye huyu huyu alimshindwa JK ambaye alikuwa anaendeleza upuuzu alioanza.
 
Back
Top Bottom