Ni ngumu sana mtu kuamini kama kuna umuhimu wa jujifunza kuhusu kujihami na kutumia mbinu hizo mbalimbali za kujilinda na fisi kwa sababu haingii akilini kwa mtu kwamba kuna siku atakutana na fisi katika mazingira hatari. Ndugu usishangae inawezekana kabisa. Mimi niliwahi kusafirisha msiba tukapita Ngorongoro lakini huko mbele ya safari tukapotea njia humo porini ghafla gari ikashindwa kupandisha milima usiku na mvua inanyesha ikabidi baadhi tutembee kwa miguuu ilikuwa hatari sana na hakuna gari iliyo karibu. Dereva alivyoona gari inapanda-panda kwa kuwa nyepesi sijui kajisahau kavuta mafuta tunakimbiza gari mpaka gari ikapotea kabisa kwenye kona kona za mlima kaenda kutusubiri huko juu. Ilikuwa hatari sana maana tulikutana na gari moja inashuka jamaa katuambia ili eneo ni hatari sana kuna mtu aliuwawa na simba mwaka jana hapa mlimani tusifanye mzaha kabisa au vipi turudi nyuma getini tujipange upya.