CHASHA FARMING
JF-Expert Member
- Jun 4, 2011
- 7,950
- 9,509
@Komandoo, haya ni sahihi kabisa katika familia na mila na desturi za kitanzania lakini sielewi ni kwanini ni tofauti na mila na desturi za kihindi na haya apply kihivi saaana katika mila na desturi zao... nimepitia kidogo literature za entrepreneurship in india inaonyesha biashara zao nyingi na kubwa ni familly owned and mostly managed by women na zaidi ya yote wanahakikisha members of the familly wanashiriki zaidi bila kujali ana mwelekeo gani na bado biashara zao zinakua.
Wakati flani nilipomaliza form four nilifanya tempo mohamed entreprise, manager was an old lady one of the supervisors was a young indian boy mvuta bangi kishenzi na akili zake alikuwa anaonyesha kabisa yuko adicted lakini cha ajabu inapokuja kwenye kazi linajituma kweli na hakuna cha wizi kinapita kwake...
Asante Chasha, yaani imefikia hadi tunatahadharishwa tuogope kuajiri ndugu kwenye biashara, shauri ya wisi na ubadhirifu, halafu hawajitumi, pia nao wanajiona ni wadau kwa hiyo nao ni viboss. Nadhani ni suala la kuwaandaa wana familia, ni suala la kufundishana na kuchuja ili kubaini wale waliona mwelekeo kuwa ajiri. Biashara zetu zinapaswa zilete neema kwa kutoa ajira kwa waliokaribu na sisi, tuwachambue wasiobebeka tuachane nao wenye uelewa tuwaelimishe na kusonga mbele! Ukweli unabaki kuwa zimwi likujualo halikuli likakumaliza. Tuwaelimishe.
AiseeDah, Hii thread nilikuwa nisha isahau, asante sana kwa kuiibua