Mjadala: Viongozi wetu wa kisiasa wapewe semina elekezi

KAUMZA

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
699
237
Tangu serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani na baada ya teuzi mbalimbali kufanywa na Mhe Rais, nimekuwa nikijionea vitimbi na vituko vinavyofanywa na wateule hawa.

Kitu nilichokibaini ni kuwa aidha hawajui au wanajua ila wanasahau.

Mfano: Kitendo cha Naibu Waziri wa Afya Mhe Kigwangalla kwenda hospitali ya Muhimbili na kufunga geti na kisha kupiga mstari ktk kitabu cha mahudhurio ya watumishi, kilikuwa ni kichekesho na kituko cha karne.

Mtumishi wa Umma ni sheria. Kuna sheria zinazomuongoza. Kanuni za kudumu za utumishi wa umma (Standing Orders 2009) zinaeleza, mtumishi anatakiwa kufika kazini saa ngapi!! Zinaeleza pia, nani anatakiwa kupiga mstari ktk kitabu cha mahudhurio ya watumishi.

Najiuliza, Naibu Waziri mamlaka yale kayapata wapi?

Kituko kingine kimetokea Mwanza. Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe Luhaga Mpina amenukuliwa na vyombo vya habari (TBC) akitoa siku mbili kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza ajieleze, kwa nini Mkoa wa Mwanza umekithiri kwa uchafu!!

Hiki ni kituko!!

Naibu Waziri, anapata Mamlaka wapi wa kumtaka Mkuu wa Mkoa ajieleze!!? Naibu Waziri kiitifaki ni mdogo sana wa mkuu wa mkoa. Naibu Waziri ana hadhi ya DC.

Kiitifaki, mkuu wa mkoa ana hadhi ya Waziri.

Nitatoa dalili

Chini ya Waziri, kuna Mtendaji mkuu wa serikali ambaye ni Katibu Mkuu (Mteule wa Rais). Na chini ya Mkuu wa Mkoa kuna Mtendaji mkuu wa serikali ambaye ni Katibu tawala wa mkoa (Mteule wa Rais).

Kiitifaki, Waziri na mkuu wa mkoa wapo horizontal.

Bila viongozi hawa wa kisiasa kupewa semina elekezi, watavuruga mifumo mbalimbali kwa lengo la kutaka sifa au kutaka uwepo wao uonekane.

Nakaribisha mjadala
 
Back
Top Bottom