Mjadala Uchaguzi wa marudio Zanzibar

mshamu

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
418
133
Nawakaribisha wataalamu na wachambuzi wa maswala ya kisiasa kutoa uchambuzi juu ya hali ya uchaguzi wa marudio Zanzibar.
Je kuna ukweli kuwa watu hakujitokeza kwa wingi kipiga kura?

Je mara baada ya mshindi kutangazwa JPM atauzungumziaje uchaguzi huo

Je ndani ya CUF hakuna mpasuko na usaliti wa makubaliano ndani ya chama.

KARIBUNI
 
Zanzibar hakukuwa na uchaguzi
Kule kulikuwa na Maigizo na Futuhi
 
asikudanganye mtu hakuna cha JPM au JMK hawa wote ni wamoja yani JPM+SHEIN= CCM waroho wa madaraka
WATANZANIA TUELIMIKE TUTADANGANYWA KILA SIKU KWA KIGEZO CHA MAJIPU hakuna lolote kama JPM yy ni ngangari afumue mikataba ya gesi na alete katiba mpya LA SIVYO HAYA YOTE NI KUSUKUMA SIKU ZIENDE
CCM NI ILEILE na hii ni serikali ya maigizo daily JPM akilala anawaza nitaonekana vip kwenye media na ya kupiga cm clouds ishachuja TUSUBIRIE KIBWAGIZO KINGINE
 
asikudanganye mtu hakuna cha JPM au JMK hawa wote ni wamoja yani JPM+SHEIN= CCM waroho wa madaraka
WATANZANIA TUELIMIKE TUTADANGANYWA NA KILA SIKU MAJIPU hakuna lolote kama JPM yy ni ngangar afumue mikataba ya gesi na alete katiba mpya LA SIVYO HAYA YOTE NI KUSUKUMA SIKU ZIENDE
CCM NI ILEILE na hii ni serikali ya maigizo daily JPM akilals anawaza nitaonekana vip kwenye media na ya kupiga cm clouds ishachuja TUSUBIRIE KIBWAGIZO KINGINE
magufuli anapumbaza watanzania wenye ufinyu wa fikra-mult nationa companies ndo wanaongoza kwa kuinyonya nchi kiuchumi kupitia mikataba lukuki frki ht hadi leo hajawai kuongelea
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Yapo ya kujadili katika uchaguzi ule.

1. Marejeo ya uchaguzi ule yalikuwa kinyume cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kwa kuwa hakuna ibara yoyote ndani ya Katiba hiyo inayompa mamlaka Mwenyekiti wa ZEC kuufuta uchaguzi wote na matokeo yake yote.

2. Uamuzi wa chama cha CUF kutokubali kushiriki uchaguzi huo wa marejeo ulikuwa sahihi kwa asilimia 100, kwa kuwa kama wangekubali kushiriki uchaguzi ule wangekuwa wanaafikiana na kitu ambacho ni batili.

3. Kutokana na Jecha kutoa matokeo yote ya Urais pamoja na Baraza la wawakilishi katika siku ya kwanza tu baada ya kumalizika uchaguzi huo wakati katika uchaguzi wa aina hiyo hiyo wa tarehe 25/10/2015, alikuwa akishikwa na kigugumizi na kutoa matokeo kwa siku 2 mfululizo na siku ya 3 akaamua kuyafuta matokeo yote.

Sasa swali kubwa la kumuuliza Jecha ni kitu gani kilichomfanya katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana awe na spidi ya kinyonga ya kutangaza matokeo na uchaguzi wa jana amekuwa na spidi ya Supersonic ya kutangaza matokeo hayo.

Kutokana na mazingira hayo ya utangazaji wa matokeo kwa dizaini ya Kijecha, watanzania kwa mara nyingine tena tumepata ushahidi usio na shaka hata kidogo kuwa Tume zetu za uchaguzi hapa TZ siyo huru hata kidogo na zinapewa 'job descriptions' na watawala kuwa wanaruhusiwa kwa nafasi ya Urais kumtangaza mgombea wa CCM pekee kuwa mshindi na si vinginevyo!
 
Hilo ndilo.suala la kujiuliza, kumbe matokeo.yanaweza kutoka ndani ya masaa 24? Zaidi ya hapo ni mbinu ya kuchakachuwa tu! Nakubaliana na wewe point 1-3. Na hii turn out ya 67+% sijui imetokea wapi?
 
Back
Top Bottom