MJADALA: Nini kifanyike kuwadhibiti madalali wa nyumba, vyumba, mashamba, gari n.k?

1. Kila mtu mzima mwenye akili timamu ana uwezo na utashi wa kuamua kutumia huduma au kuacha. Hii inahusika pia na kwenye huduma ya udalalali.

2. Sheria zilizopo zinatosha kabisa kushughulika na madalali. Hakuna sababu ya kuanzisha urasimu mwingine, kwani huko ni kuongeza ukubwa wa serikali kusiko kwa lazima.

3. Sera za Ruksa (Small governments, individual responsibilities and freedoms) mara nyingi huhusika na maendeleo.


Government's view of the economy could be summed up in a few short phrases: If it moves, tax it. If it keeps moving, regulate it. And if it stops moving, subsidize it.

Ronald Reagan Quotes
 
1. Kila mtu mzima mwenye akili timamu ana uwezo na utashi wa kuamua kutumia huduma au kuacha. Hii inahusika pia na kwenye huduma ya udalalali.

2. Sheria zilizopo zinatosha kabisa kushughulika na madalali. Hakuna sababu ya kuanzisha urasimu mwingine, kwani huko ni kuongeza ukubwa wa serikali kusiko kwa lazima.

3. Sera za Ruksa (Small governments, individual responsibilities and freedoms) mara nyingi huhusika na maendeleo.




Ronald Reagan Quotes
Point namba 1 ni ngumu sanaaa. Wenye nyumba ukiwafata wanakataa kukupangisha bila dalali. Na wao hawaumizwi na madalali bali ni sisi wapangaji.
 
Usiwe na wasiwasi, sheria IPO mbioni kwenda bungeni. Inaundwa mamlaka kama ilivyo Ewura, Sumatra. Hiyo mamlaka itasimamia shughuli zote zinazofanywa na madalali. Madalali wajiandae, manake leseni zitatolewa na mamlaka hio.
 
Udalali unarahisisha kupata hitaji husika wakati husika. Waulize Credit Suise watakufafanulia namna ya kukopa.
 
Kumkomesha Dalali Ni Sawa Na Kumaliza Tatizo La Ufisadi Tanzania
HEbu Waite Waliosoma Masuala Ya Uchumi Na Kisha Ujue Ya Kuwa Dalali Ni Nani na Anahusika Vipi KAtika Biashara
Point Ilitakiwa Iwe Wanatakiwa Kusajiriwa
Ili Wafuate kanuni Halali Zinazokubalika Kisheria
Mfano Labda Hatakiwi Kuongeza bei ila Atachukua Asilimia 8 au kadhaa katika Mauzo Yake
Kudhibiti ni Kuweka Wawe Wanasajiliwa na Serikali Na Kufuata kanuni Maalum.
 
Ingawa mtiririko wa hoja yako hauna maaana kimantiki kuhusiana na hoja iliyopo mezani ngoja nijibu hoja yako.

Sioni kwamba wakifanyacho madarali ni 'uovu' pengine utupe tafsiri ya neno uovu kwa muktadha uliopo. Lakini pia ukishasema naweza kutetea mafisadi kwa kuiba pesa za umma. Unafananisha wizi na udalali unafanya makosa makubwa sana, wizi ni jinai na udalali ni huduma. Sifa ya huduma inaweza kuwa nzuri kwa mtu mmoja na ikawa kero kwa mtu mwingine. Kitu cha msingi ni kujaribu kuishauri Serikali kupitia Serikali za mitaa kuratibu shughuli za hawa madalali ili iwe chanzo cha mapato kwa serikali kutokana na kulipa kodi kwa huduma zao lakini pia kuwe viwango sawa kwa huduma zao.

Hakuna sehemu duniani kusipokuwa na madalali. Jiulize leo, Serikali ingekuwa inakusanya kodi za maegesho yenyewe bila kutumia madalali ingekuwaje?, fikiria mimi nipo busy na majukumu nataka chumba, nyumba, shamba n.k sehemu ambayo sina uzoefu nayo bila msaada wa hawa madalali inakuwaje?
Hivi bado mnamda wa kubishana na huyu Mr.Zero...?
 
We
Anakuambia hivi kwakuwa hukuitafuta nyumba mwenyewe Ila kwa msaada wa dalali....

Kama ndivyo basi inakubidi utumie the same way uliyoitumia mpaka ukaijua nyumba...


kama uliijua nyumba mwenyewe bila dalal je dalali anahusikaje hapo..?

Tafuta nyumba, kiwanja peke yako alafu uone kama dalali atahusika...utarelaksi rafiki na wala hutalalamika kama ulivyobwabwaja hapa....

Ila kama uliona peke yako huwezi pata nyumba,kiwanja....na ukaona iliuweze kupata kirahisi ni mpaka umtumie dalali...pasi shaka itakubidi umlipe dalali ndugu yangu...

Hivi unajua madalali wakikunununia hatakama una nyumba 10 bora kabisa itakuwia ugumu kupata wateja...?

Au tufanye unauza kiwanja/shamba 50km from city center...na unahitaji wateja...je mteja aliyeko njombe mji atalala na kuota kuwa kuna shamba unauza...?
Au dalali atachoma mafuta kutoka alipo kuja kuhakikisha unachouza ni sahihi na kuthaminisha......je mafuta anayotumia dalali mpaka huko assets zilipo analipwa nanani...?


Hivyo unapaswa kuwaheshimu madalali mkuu...evenzou huoni uwajibikaji wao kwa unachohitaji......


Ukienda kwa mwenye nyumba direct hakubali...anakuambia madalali watamletea shida
 
Kwa kweli madalali ni shida. Ila mda wao unakaribia kuisha.Tumieni KUPATANA achananeni na madalali.
 
Habari wakuu,

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu, kumekuwa na changamoto kubwa katika suala zima la kupanga na kununua nyumba, mashamba, magari na kadhalika.

Hawa watu wanaojulikana kama madalali au 'mtu wa kati' wamekuwa wakifanya maisha kuwa magumu kila siku yaani ni kero kwa kifupi. Hawana huruma hata kidogo, imagine nyumba inauzwa milioni 20 yeye atataka akuuzie milioni 50.

Kwenye vyumba ndo usiseme kuonyeshwa tu 10,000/= haijalishi utaipenda ama vipi. Ukishaipenda inakubidi umlipe malipo ya mwezi mmoja tena hawapunguzi hata 100/=.

Mbaya zaidi hawalipi kodi wala mapato yao hayana msaada wowote kwa nchi na jamii kwa ujumla zaidi ya kuwaumiza wananchi.


Je, unafikiri nini kifanyike kuwadhibiti?
Wakamatwe tuu
 
Kuna hawa jamaa wanaitwa Pangisha. Inaonekana wata-transform upangishaji wa nyumba. Wanadai kidogo tu na si kodi ya mwezi mzima halafu mteja kweli akipanga nyumba watamrudishia ile fedha aliyotoa ya kumzungusha maana wateja wengine huwa wanataka nyumba halafu mwisho wa siku wanapotea.

Pangisha
 
Nyie ndio mnao waendekeza,kuna nyumba aliipenda brother wangu ilikua tshs 800,000/month,dalali akamwambia atachukua kodi ya mwezi,bro akasema nipeleke nikaione kwanza,dalali kapewa 20,000 tukaenda kuicheki nyumba,kisha tukamwambia mpigie mwenye nyumba aje asbh,kesho yake bro baada ya kuonana na mwenye nyumba akamwambia atalipa hiyo 800,000x18months=14,400,000..kisha akamwambia dalali kwamba atampa laki tu bcoz pesa aliyonayo ni 14,500,000 pekee,kama hataki basi ataachana na hiyo nyumba,mwenye nyumba kusikia hiyo mihela akasema nyumba ni yangu na dalali hajui ata nikitumia tofali ngapi so twende sehemu husika nikupe mkataba unipe pesa,dalali hakua na namna zaidi ya kukubali hiyo 100,000!!
HUYO SIO DALALI WA MJINI,KAKA YAKO ANGEKUWA NAIROBI SAA HII
 
From my point of view!!!hivi vinatokea kwa sababu hakuna sheria na utaratibu!!! Kinachotakiwa ni
1. kuwe na tume inayowaregulate madalali na isajiliwe serikalini
2. kila dalali asajiliwe kwenye hyo tume na agewe leseni
3. Kuwe na sheria itungwe kabisa ambayo itaregulate na kucontrol hii biashara ya udalali na itengenezwe kabisa comission structure
Tukifanya hayo itasaidia sana hii inshu za watu kutapeliwa na kuover price items na kuondoa kuondoa all other unnecessary costs.
 
Yaani hawajamaa madalali ni wezi kama wezi wengine tu na wanaleta kero kwa jamii sana, na chakushangaza kwanini wanapenda sana pesa kuliko kutoa huduma ipaswavyo, alafu pia hii kitu yakusema eti akikupeleka kuona nyumba shamba kiwanja nk basi umpe nauri, je kazi yake inaweza kukamilika kama hajammuonyesha mtema eneo au nyumba? Je jukumu la kumuonyesha mteja bidhaa ilipo niyanani? Kwasababu kwa ukweli hawa jamaa ni kero sana kwenye jamii alafu pia kodi hawalipi wala nini , utakuta umekwenda kwa dalali unahitaji huduma anakwambia umpe nauri, unamwambia nina gari yangu twende bado anataka umlipe , hii haiko sawa jamani na hili jambo lapaswa kupingwa na kufabyiwa maandamano makubwa tu kama mambo mengine yanavuo pingwa nakufabuiwa maandamano nchini
 
Asanteni Jamii forums kwa kuipa thread yangu kipaumbele,nashukuru wadau wote pia kwa michango yenu hakika nimejifunza kitu...kumbe ni wengi tunasumbuliwa na hawa jamaa
 
Back
Top Bottom