Mjadala: Kwanini watoto wa kiume wazawa wa Dar wanapenda mambo ya kike....???

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
19,166
37,176
Habari za wakati huu wandugu na majamaa.....

Katika pita pita zangu mjini hapa nimekumbana na vituko vingi sana ambavyo naweza kusema ni vya kawaida sana kwa maisha ya mjini...lakini kinachonishangaza na kunistaajabisha ni tabia ya watoto wa kiume wa dar hasa wale ambao ni wazaliwa hapa Dar kuwa na tabia zinazofanana na dada zao....kama wenyewe wanavyojiita wandewa...

Ni nadra sana kukaa vijiwe vilivyojaa wazawa na kupata au kusikia maongezi ya kupambana na maisha kama vile kubuni miradi mbali ya kukuingizia kipato......au harakati na mipango ya maendeleo zaidi ya kupata ratiba za maeneo ya starehe za mji mzima huku wakiwa wananukia kama wanawali wanaongoja kuolewa....bila kusahau ukikaa nao utapata habari za watu wote maarufu hapa mjini....kuanzia vipato vyao mpaka maisha yao binafsi......

Hali ni hivyo hivyo hata kwenye vikao vya dada zao......

Uvaaji wa nguo za kubana na kuonesha makalio yao pia na kuvaa heleni masikioni inawafanya marijali washindwe kuwatofautisha na dada zao...tena kuna wengine wameenda mbali zaidi maana mpaka wanasukana na dada zao vibarazani....

Mara nyingi huwa najiuliza kwanini inakuwa hivi au ndio utaratibu wa maisha ya pwani na wazawa wote wa mjini....???

Nawasilisha.....
 
Back
Top Bottom