Mjadala: Je, ni siku zipi ambazo mwanamke huweza kupata ujauzito katika mzunguko wake wa kila mwezi?

saladi

Member
Dec 4, 2012
31
11

MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU:
Habari wana JF,

naomba kuelezwa ni tarehe zipi ndani ya mwezi naweza fanya mapenzi na mke wangu bila kutumia kinga na asipate ujauzito.

Natanguliza shukrani kwa watakaonipa majibu.
===
===
===


MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU:
-----
-----
-----
 
Hesabu siku ya 11 -15 toka uanze bleed ..hizo siku ndizo za kupata mimba.. Kwa wewe kwa mujibu wa tarehe ulinzo weka hapo.. Siku ya kupata mimba ni kuanzia tarehe 13-17 dec...

Kwa hesabu za urahisi unaanza hesabu siku 10 toka tarehe ya kuanza bleed kwa hiyo kunazia siku ya 11 hadi 15 ndizo siku za kushika mimba kwani yai la uzazi linakuwa tayari limeshuka linangoja kurutubishwa na mbegu za kiume
 
kaka umeeleza vizuri sana lakini kuna dr alinambia kuwa yai huwa inaenda mpaka siku ya 17 hv! unajua wanawake wengi sana huwa hawajui siku zao za hatari wengi wao wanajua ni kile kipindi cha mp
 
thanks kibe na zema, nitawapa matokeo, coz ndoto ni kupata mtoto,please pray for me guys.
 
Kabla ya kukwambia siku ya kupata mimba, kwanza inabidi useme mzunguko wako ni wa siku ngapi..!!
 

NIMEIKUTA MAHALI HII

Kwa mwanamke mwenye mzunguko wa kawaida wa siku 28. Yai la mwanamke hupevuka (ovulation) siku ya 14 baada ya bleed na likikutana mbegu ya kiume siku hiyo hutunga mimba (nyege huwa kali na uteute kuwa mzito unaovutika).Pia kunauwezekano pia wa kushika mimba siku 3 kabla ya yai kupevuka au siku 3 baada ya yai kupevuka, yaani kuanzia siku ya 11 mpaka siku ya 17 baada ya bleed. Kwakuwa mbegu za kiume huwa hai ndani ya uke kwa siku 3 tu (masaa 72) kabla ya kufa na Yai lamwanamke hukaa siku 3 tu (72hours) likisubiri mbegu za kiume kutunga mimba kabla ya kufa. Uki sex siku ya 11 mbegu zitakuwa bado active kwenye uke kwa siku 3 na kulikuta yai siku ya 14 ya kupevuka kwake hapo mimba hutungwa.Na iwapo pia ukisex siku ya 17 ambapo ndio siku ya mwisho ya uhai wa yai kusubiri mbegu za kiume hapo mimba hutunga.
Kwa wale wenye siku zinazobadilikabadilika (22, 24, 26, 30) kutokana na stress, vyakula,madawa, maradhi au mshituko ili kutafuta mtoto mnashauriwa kusex siku 7 kabla ya yai kupevuka, siku ya yai kupevuka, hadi siku 7 baada ya kupevuka. ila kwa uhakika wa kutopata mimba ni kusex kuanzia siku ya 17 hadi siku moja kabla ya bleed.
 
kaka umeeleza vizuri sana lakini kuna dr alinambia kuwa yai huwa inaenda mpaka siku ya 17 hv! unajua wanawake wengi sana huwa hawajui siku zao za hatari wengi wao wanajua ni kile kipindi cha mp


siku ya 17 mara nyingi sana hukana mimba ..ingawa sina uhakika sana mana kuna wanawake wengine muda unakuwa mrefu inawezekana ikafika hapo siku ya 17 ingawa ni mara chache sana
 
Nashukuru kwa maelezo mazuri.

Je kwa wanandoa ambao wana kiu ya kupata mtoto wa kiume au kike siku zipi ni muafaka kukutana kwa kina mama ambao vipindi/siku zao hazibadiliki.


Ahsante
 
kwanza badilisha tittle yako,nilifikiri siku ya kushika mimba kitaifa.ushauri wangu,daktari anaweza kukusaidia ,unaweza kuwa na matatizo mengine zaidi na sio swala lako la timing tu.nenda kwa dr gynaecologist
 
Nashukuru kwa maelezo mazuri.

Je kwa wanandoa ambao wana kiu ya kupata mtoto wa kiume au kike siku zipi ni muafaka kukutana kwa kina mama ambao vipindi/siku zao hazibadiliki.
Ahsante
Mtoto wa kike: Hesabu siku tatu za mwanzo yaani siku ya 11,12 na 13 baada ya PM na
mtoto wa kiume: hesabu siku tatu za mwisho yaani siku ya 14,15 na 16 au 17 baada ya PM

Josam
 
Mtoto wa kike: Hesabu siku tatu za mwanzo yaani siku ya 11,12 na 13 baada ya PM na
mtoto wa kiume: hesabu siku tatu za mwisho yaani siku ya 14,15 na 16 au 17 baada ya PM

Josam
Uko sawa; ila inategemea na mume anatoa mbegu gani?!
 
Just relax bi dada enjoy the moment with your special one na mambo yatajipa lakini ukijipa pressure kiasi hicho basi unaweza kurefusha zoezi la kupata mimba kuliko inavyostahili. Good luck and all the best.

jamani nimebleed tarehe 3/12/2012 hadi tare 9/12/2012 ni siku gani naweza kushika mimba.
msaada pliiiiiiiiiiiz maana huwa inasumbua kila nikijaribu hola
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…