MITANDAO YA SIMU KWA HILI MNATUUIBIA

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
831
1,595
Na Bollen Ngetti
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania Limited, hiki mnachokifanya ni wizi na unyang'anyi kama ulivyo ukabaji, kuvunja nyumba ya mtu na kumuibia au kumpora Mali yake kwa nguvu na hata kumjeruhi au kumuua. Kinachotia hasira na hasara zaidi ni kuona TCRA wanajua wizi na utapeli huu lakini wakijifanya kutoona au haiwahusu. Wanashiriki wizi na utapeli huu wa VODACOM. Shame indeed!

Iko hivi, katika huduma zenu za vifurushi mtu ananunua "bundle" la Tsh 1,000.00 mnampa MBs 200 mkiita za saa 24. Kwamba saa 24 zikiisha basi MBs 200 zinakuwa zimeisha. Wizi mnaufanya pale ambapo mteja hakutumia huduma ya internet (data) au katumia kidogo mno. Lkn saa 24 zinapofika tu, tayari mnambania pua, "Ndugu mteja kifurushi chako cha internet kimekwisha, kununua piga *149*03#" Mimi nimeshanunua bidhaa kutoka kwako, Bando ambayo sasa ni Mali yangu halali maana hata risiti umenipa, kwa nini unipangie muda wa kutumia Bando langu? Kwani nikishanunua kifurushi kwenu bado kifurushi hicho ni Mali yenu hadi mnipangie namna ya kuitumia? Huu ni wizi! Msinipangie muda wa kutumia unless ni kifurushi cha bure lkn si niliyonunua kwa hela yangu. Mkome!
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]!

NOTABENE: Napenyezewa hapa kwamba si Vodacom pekee Bali makampuni karibu yote ya simu yanashiriki ujambazi huu na Rais JPM anatazama tu wanyonge wanavyonyongwa. TCRA mjipime.
 
Ndio maana saasa imekuja na haina kikomo..lkn by the way..ukiona vp usijiunge utumie pesa yako moja kwa moja ndio utaona una saidiwa saana..
 
Back
Top Bottom