Wana bodi, nchi ndio maana ina mikosi mingi, haisogei. Tatizo ni watunga mitaala, wasimamizi na watendaji wetu.
Leo wife ambaye anafundisha darasa la tano geography, kaniomba nimsaidie kusahihisha mitihani ya kumaliza muhula darasa la tano geography.
Sasa nimepewa marking scheme, hivyo natakiwa nisahihishe kuifuata. Ila pepa ya kwanza nasoma swali kwa swali na nalinganisha jibu halisi na lililo kwenye marking scheme.
Nimeshtushwa kwenye swali kuwa, "Africa mashariki imeundwa na nchi_________
(a) Tano
(b) kumi
(c) mbili
(d) tatu.
Watoto wamejibu d) tatu, hivyo aliyejibu tano anatakiwa apewe kosa.
Hivi wizara ya elimu mmekuwa mkifumdisha watoto wetu upuuzi huu tangu 2009 hadi leo 2017 kweli?
Yaani hadi sasa wizara ya elimu hamtambui kuwa Rwanda na Burundi ni wanachama hai wa africa mashariki?
Yaani hata wabunge na maspika waliotoka burundi na rwanda kwenu walikuwa wanapoteza muda wao kwenye afrika mashariki?
Aisee, nchi yetu inaumwa sana, tena sana. Tuliko fika ni kubaya zaidi.
Sasa natamani waliojibu tano niwape vema na waliojibu tatu niwalime. Lkn ntakuwa nimewaonea, siyo kosa lao. Vitabu vyao vinawaelekeza hivyo.
Majanga.