Mistake!:: Kosa kubwa la mkuu wa kaya

Mistake!:: Kosa kubwa la mkuu wa kaya

Manmura

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
750
Reaction score
169
Moja ya mambo ambayo serikali yetu ya mheshimiwa jk kufanya ni hili la kupeleka wanajeshi kuwa walizi wa raia na Mali zao baadala ya kuwa walinzi wa mipaka ya nchi haya mahusianao kati ya jeshi na wananchi hayapaswi kufumbiwa macho hata kama wamepelekwa kulinda maslahi ya viongozi wetu ... Hii hali tuliizoea kwa polisi kutumiwa na viongozi wetu kwa maslahi binafsi na sasa wameingia mkenge kwa kutumia jeshi bila kujua mathara yake baadae kwa taifa hususani nidhamu jeshini na mambo mengine mengi ,, hapa walichokiangalia zaidi viongozi wetu ni maslahi yao binafsi na sio ya taifa ... Kumpeleka mwanajeshi kulinda interest zenu huu ni kujiondlea hushima kwa wanajeshi na hatari yake ni kuwa kutokana na ukweli kuwa na wenyewe ni binadamu na ukweli wa mambo wanaujua,,,siku wakielimika??? Ni nani amulaumu mwenzake??? Mm naishauri serikali iendelee kuwatumia polisi kama ilivyozoea na sio jeshi hapa ni kujimbia kabur ww mwenyewe bila kujua,, hawa watu wamezoea kukaa porin bila interaction na watu huduma za nchi za manunuzi in short hawana hardness ya maisha kivile sasa hii ya kuwachanganya na raia ile hali wametoka uraian ni kuhatarisha amani ya nchi,,, polis huogopa kugeuka serikali kwa vile wanajua mziki wa wanajeshi,hii ya kuishi na raia siku uzalendo wa hali ngumu ya maisha ukiwaingia sijui itakuweje!! My take!.:... Serikali rudisheni mara moja hawa wanajeshi wa mtwara kwenye kambi zao husika,,,,,,, wabunge lionani hili nchi yetu,,, amani yetu tunaipenda sana...
 
Jwtz ilipaswa wafanye kazi hiyo mkoa wa mara tarime!
 
WanaJeshi nao ni Watanzania wanajukumu la kulinda amani ya Nchi ndani na nje ya mipaka yetu, Kuijenga nchi (Mafuriko, Madaraja, kutibu wagonjwa nk) kushiriki shughuli zote (Kupiga kura, kutoa damu na huduma kadhaa)
Ndio maana kila mtanzania anashauriwa apitie JKT aua hata Mgambo mambo km haya asingeyauliza.
Kwa jinsi nilivyomuelewa mtoa Mada ni kuwa kimemuuma kuwa Wana Mtwara wametulia na kuuona ukweli sasa wamejitenga na uchochezi.
Mbona wameenda DRC kwa Kabila, hukulalamika,
mbona waliingia Mitaa ya Kariakoo hukulalamika,
Kuwanyamazisha walioleta vurugu Mtwara ndio kimekukera ulitaka ushangilie Fujo na kulipuwa majengo magari na watu?
 
Acha walinde amani bwana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
uko sahihi mr, police wa nini kama hawawez kutimiza majukumu yao.
 
umekalili kuwa kazi ya jesh nikulinda mipaka tu.ukitibiwa na wanajeshi huwa mnashukuru,pitia majukumu ya jeshi ktk katiba ya nchi yetu yapo wazi.
 
WanaJeshi nao ni Watanzania wanajukumu la kulinda amani ya Nchi ndani na nje ya mipaka yetu, Kuijenga nchi (Mafuriko, Madaraja, kutibu wagonjwa nk) kushiriki shughuli zote (Kupiga kura, kutoa damu na huduma kadhaa)
Ndio maana kila mtanzania anashauriwa apitie JKT aua hata Mgambo mambo km haya asingeyauliza.
Kwa jinsi nilivyomuelewa mtoa Mada ni kuwa kimemuuma kuwa Wana Mtwara wametulia na kuuona ukweli sasa wamejitenga na uchochezi.
Mbona wameenda DRC kwa Kabila, hukulalamika,
mbona waliingia Mitaa ya Kariakoo hukulalamika,
Kuwanyamazisha walioleta vurugu Mtwara ndio kimekukera ulitaka ushangilie Fujo na kulipuwa majengo magari na watu?

naunga mkono hoja, alivotaka "nchi isitawalike"!
 
Back
Top Bottom