sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,487
Namwonea huruma mama wa watu asubuhi amewaambia watoto wake kuwa "wanangu leo tutakula vizuri" akatoka akaenda kazini, amerejea mchana hana amani salio bado halijasoma na ikabidi wapike uji wa chumvi maana sukari nayo ni shida, na muda wote wanasubiri ujumbe wa NMB Mobile bila mafanikio. Sidhani kama jioni kuna ujanja wowote wa kubadili mlo.
Suala ni kwamba watumishi wa Umma hususani walimu wanalipwa mshahara kidogo wenye makato mengi na mwisho wa siku kile kinachoingia kwenye akaunt yake hakiwezi kumtosheleza kumudu gharama za maisha kulingana na bei ya vitu.
Mfano chukulia mwalimu anayepata mshahara wa 520,000/= halafu makato yanakuwa hivi: P.A.Y.E 9%, PENSION 5%, CWT 2%, BIMA 3%, KAMA ANATOA ZAKA, 10%, jumla ni 29%. Anabakiwa na 370,000/= hapo ukute ana kamkopo bank hata 50,000/= anakatwa moja kwa moja. Atabakiwa na 320, 000/=. Tufanye kodi ya nyumba, umeme, maji na nauli ya kwenda shule kwa kujibana ni 100,000/=, anabakiwa na 220,000/=. Hslb wanamkata 60,000/=
Hii pesa ambayo haifiki hata posho ya mbunge kwa siku moja ya sh 160,000/= huyu mwl mwenye watoto wawili ataishije na watoto kwa mwezi mzima? Bado mwisho wa mwezi wenyewe pesa inachelewa? Hawa wabunge kazi kudai bunge live badala waangalie maslahi mazuri kwa wananchi?
Serikali ni vema iangalie upya mishahara ya wafanyakazi na hayo makato yasiyo na maana yaondolewe mfano bima na pension isizidi 1%.