sonofobia
JF-Expert Member
- Jun 21, 2015
- 1,167
- 4,287
Habari zenu wadau, Plz msichoke kusoma ili gazeti.
Nakuja tena kwa mara nyingine kupata ushauri wenu na uzoefu maana umu kila mtu kapitia hali fulani na akaikabili kwa namna yake.
Nilikuja umu bandiko namna ya kumwambia ukweli mpenzi wangu kwamba nampenda ila sitokuja kumuoa. Kila mtu alinipa ushauri wake ila wengi wakanishauri nimweleze tu ukweli kuwa hatuna future nae ili akae akijua.
Wengine wanaweza kuhoji kwa nini nimpende mtu alafu nisitake kumuoa. Ishu kubwa sio elimu kama wengi walivyojaji japo huyu mpenzi ni kweli elimu yake ni ndogo ila kikwazo ni kwamba tayari mwenzangu ana mtoto na sikujiandaa katika maisha yangu kuoa demu mwenye mtoto. Ata nikijaribu kupata ushauri kwa ndugu jamaa na marafiki wengi hawaungi mkono mimi kuoa msichana mwenye mtoto .
Leo nimekuja kuomba mawazo yenu wadau, maana baada ya kumwambia ukweli huyu msichana. Aliumia sana na kulia kila siku lakini baadae akakubaliana na matokeo mapenzi yakaendelea vizuri.
Sasa hali ikaanza kubadilika wiki moja iliyopita akawa mzito kila kitu, akawa anafanya mambo yake bila kunishirikisha yani akabadilika kwa kweli.
Juzi mchana tumeongea vizuri akaniomba ushauri kuwa kuna mtu amejitokeza anataka kumuoa na yupo tayari kufata process zote ila yeye kama yeye hampendi. Nikamshauri afate moyo wake unasema nini. Akasema hajisikii kuolewa nae.
Basi baadae usiku nikampigia simu mara nyingi akupokea, nikadhani anatatizo nikaenda kwake nione kuna nini, kufika kwake alipopanga nikakuta yupo macho nikagonga mlango wa chumba chake akufungua nikagonga sana akufungua. Nikahisi labda yupo na mwanaume ndani nikachungulia nikamwona peke yake ila ataki kupokea simu wala kufungua.
Mimi kwa hasira nikaondoka na kumwambia huo ndio mwisho wetu na asije nitafuta na kuniomba msamaha kama kawaida yake. Nikaondoka.
Cha ajabu na sikuwa nimetarajia siku ya pili sasa hajanitafuta kuomba msamaha. Hakutaka nieleza kwa nini alifanya vile. Hajalalamika kwenye status za whatsapp kama kawaida yake. Kifupi kwake ni kama hakijatokea kitu ambayo Sio kawaida yake huyu demu ananipenda sana ilo sina mashaka nachoshangaa huu ujasiri kautoa wapi wa kunipotezea.
Kingine mimi sasa ndio napata shida maana naanza kuhisi kama napata homa sio homa, moyo unauma sana kama kidonda sio kawaida. Kifupi nahisi maumivu makali sana sana.
Nimeshaachana na wanawake tofauti hapo kabla ila sijawahi jisikia hali ya namna hii. Nipo njia panda kwa kweli maana nimegundua nampenda sana ila sijui nifanyaje.
Naombeni mawazo yenu wadau. Naombeni mawazo yasiyoongozwa na huruma bali uzoefu wenu.