Mimi napenda mfumo dume' wewe je?

High % of divorce rate,usagaji na ushoga ni matokeo ya "mfumo wa usawa" enzi za mfumo dume haya makitu halikuwa hakuna.
 
Mfumo dume wazee wetu waliuweza kwa sababu kila kitu mzee alikuwa anahudumia na kusimamia. Lakini vijana wa leo wanachangia kununua chakula cha nyumban na mkeo halafu unataka mfumo dume. Mtashikwa mno masikio, si wanawasaidia matumizi.
 
Mfumo dume wa zamani ni kweli ulidumisha ndoa lakini haukutokeza ndoa zenye furaha na amani. Unajua amani si ya kimwili tu bali pia ya kiakili na kihisia. Wanawake nyakati hizo waliwekwa katika tabaka la chini kama watoto. Mke alipokea tu amri kutoka kwa mume na kutekeleza hangeweza kutoa maoni tofauti ili mume ayatafakari na kuyapima kama yanafaa. Mke kutoa tu wazo tofauti na la mumewe bila kujali kuwa alilitoa kwa unyenyekevu pengine akiwa amepiga magoti tendo hilo lilionwa kama kukaidi mamlaka ya mume. Mke angefokewa na hata kupigwa. Mke alionwa kama mtumwa wa mume. Mke wa wakati huo twaweza kumfananisha na housegirl anayetekeleza maagizo tu ya bwana mkubwa. Kuolewa kwenyewe kulifanyika kibabe. Mwanaume alipompenda msichana mipango ya ndoa ilifanyika blla binti kujua anaolewa na nani hadi siku ya arusi alipelekwa kwa mwanaume asiyemfahamu!.
Kwa hiyo twaweza kusema unyenyekevu wa wanawake ulitokana na woga na sio upendo kwa waume. Mifumo ya kijamii siku hizo ilimkandamiza mwanamke na mtoto wa kike hata kwenye masuala ya msingi kama chakula. Chakula kizuri kilikuwa ni cha wanaume. Nwanamke hawezi kukaa na kula na mumewe. Mume ale kwanza kisha mke na watoto wafuate kula. Hatuwezi kusema wanawake walikuwa na huzuni siku zote. Tutambue kuwa hayo ndio aina ya maisha walioyakuta na hivyo ujinga uliwafanya hata pale wanapoonewa waone sawa tu. Lakini wote tumezaliwa na uwezo wa kutambua lililo kosa na lililo sahihi(conscience). Kwa hiyo maonezi yanapozidi kitu fulani kinakwambia kuwa hapa sio sawa na utaumia lakini huna jinsi inabidi uvumilie.
Kwa hiyo amani katika ndoa inayotokana na ujinga na ukosefu wa uhuru hatuwezi kusema ni mfano wa kuigwa.
Kama wengine walivyosema, mume ni kichwa cha familia na mwamuzi wa mwisho katika masuala ya kifamilia. Lakini mume muelewa na anayempenda mkewe na kumheshimu kazima atamtaka mawazo kabla ya kufanya maamuzi ya kifamilia. Kwa sababu mume wa namna hiyo anatambua kuwa mke ni rasilimali(resource) muhimu ya familia maana naye anazo akili na anaweza kutoa wazo ambalo mume hakuwa nalo na likaonekana ni lenye kufaa kuliko hata lile mume aliliwazia. Mke akishirikishwa atajihisi kuwa ameheshimiwa na itachangia furaha katika ndoa.
Kwa hiyo mume kichwa- ndio lakini lazima mke ashirikishwe.
 
Am okay with mfumo dume as long as i will always remain a woman in it
 

Upo sahihi kiasi chake! ila maana halisi ya mfumo dume sio kumfanya mwanamke mtumwa kama haya maelezo yako.
 
High % of divorce rate,usagaji na ushoga ni matokeo ya "mfumo wa usawa" enzi za mfumo dume haya makitu halikuwa hakuna.

Nakubaliana nawewe 100%! Very correct!
 
Mfumo dume wazee wetu waliuweza kwa sababu kila kitu mzee alikuwa anahudumia na kusimamia. Lakini vijana wa leo wanachangia kununua chakula cha nyumban na mkeo halafu unataka mfumo dume. Mtashikwa mno masikio, si wanawasaidia matumizi.

Very true! wasahau kabisa! mwanamke akishakuwa ndiye bread winner we mwanaume kaa chini ukune nazi, uoshe vyombo na kupiga deki tu! Hakuna mfumo dume kama wewe mwenyewe ni jike ndani ya Nyumba!
 

Wanawake wangapi wana uelewa na kujitambua kama wewe! Wengine ukiwapa nafasi kama hiyo anaweza kukupanda hadi kichwani.
 
Very true! wasahau kabisa! mwanamke akishakuwa ndiye bread winner we mwanaume kaa chini ukune nazi, uoshe vyombo na kupiga deki tu! Hakuna mfumo dume kama wewe mwenyewe ni jike ndani ya Nyumba!

Utatakaje mfumo dume wakati unahudumiwa na mwanamke? Ukiona hivyo ujue hujitambui.
 
Vijana wetu wasasa lazima wote waangukie kwenye mfumo jike!

Kwasababu wanapenda maisha mazuri na kujishughurisha hawataki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…