Mkuu hapo pana tatizo, amekwisha olewa yeye ni mke wa mtu sasa, na kumgusa mke wa mtu ni dhambi kubwa. Tafuta mwingine wa kwako. By the way ... umesema "uliyempenda kwa dhati", kama ulimpenda kwa dhati mbona kaolewa na mwingine? Je, Yeye pia alikupenda kwa dhati? No, hapo pana shida mkuu, kama alikupenda kwa dhati pia asingeolewa na mtu mwingine. Epuka sana upendo wa upande mmoja.
Wanawake wapo wengi sana, utampata mwingine mtakayependana kwa dhati, na ukimpata, oa, usifanye "uasherati".