Mimi naamini kila dhambi lazima uilipie

Beesmom

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2022
Posts
37,420
Reaction score
92,254
Mi naamini kila dhambi lazima uilipie, ulipaji unaweza chelewa ila lazima muda ufike uwajibike.

Usichopenda kutendewa usimtendee mwenzio. Usipende kuvuruga amani ya moyo ya MTU Mwingine kwa kumkomoa tu huku wewe ukiendelea kuenjoy.

Unadanganya kibiashara, kifedha, kifamilia, kijamii na kimapenzi, pesa unakopa hulipi, unafanya biashara na MTU unadhurumu, unadanganyia pipi na kutishia visu watoto unawabaka, unamwahidi kumwoa unamwachia mimba unasepa, unaua wazazi kwa tamaa za mali.

Unatelekeza familia sababu ya anasa, unamwaminisha MTU mpo safari moja kumbe umeaminisha wengi-wastage of time(hili limenipata but time will tell). Karma is real tusipojirekebisha wapendwa.
 
Be patient.... Time will tell mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…