Juzi nilisikia kamishna TRA wakidai watanzania milioni 3 kati ya milioni 45 ndio wanaolipa kodi. Ni jambo ambalo halikubaliki tena kauli hii inapotolewa na wataalamu wa kodi inasikitisha maana kauli hii ingetolewa na layman.
kila mtanzania analipa kodi ila kwa viwango tofauti.
kodi nyingi zimewekwa katika bidhaa hivyo kila mtu anaponunua bidhaa hulipa kodi.
sio haki kuwalinganisha watanzania katika PAYE wakati mapato yao ni tofauti.
kila mtu analipa kodi kulingana na anavyopata, hivyo hatua ya kwanza ni kupata kama hatuwezi kusikitika kuwa watanzania wanaopata vipato vinavyowawezesha kulipa kodi ni wachache hatustahili kulalamika kuwa wanaolipa ni wachache.
hivi kiongozi anayesimama kulalamika jambo kama hili kwanza ajiulize analipwa shilingi ngapi? alafu ajiulize ni watanzania wangapi wanaolipwa kiasi hicho anacholipwa yeye?
msingi wa kulipa kodi ni kupata hivyo kujiuliza tunatakiwa tuanzie kwenye vipato ili tuwawezeshe watanzania kupata fedha na ndio hapo wakishapata tujiulize kama wanalipa. hatuwezi kusikitikia kulipa kodi kama hatusikitikii watanzania kupata vipato duni.
wakati awamu ya tano imeingia madarakani kwa viwango vilevile vya kodi kwa kubana mianya ya ukwepaji kodi waliweza kupandisha ukusanyaji mapato kwa zaidi ya asilimia 60. lakini walipotengeneza bajeti walibadilisha viwango vya kodi na kuondoa vyanzo vingi vilivyokuwa vikiingiza mapato kwenye jamii na kuzunguka kutengeneza kodi.
watu wamelalamika lakini badala ya kusikilizwa na kutafakari hatua walizozichukua wao na kuangalia biashara hizi zinazozalisha kodi zimeathirika vipi, wamewajibu wananchi walizoea fedha ya bure. Lakini cha kusikitisha ni pale wanapoonekana kutegemea kukusanya kodi zilezile kwenye biashara chache zinazofanyika.
kugangania kukusanya kiwango cha kodi kilekile ni sawa na kumtwika mgonjwa mzigo bila shaka itakuwa ni kumuongezea machungu.
wataalamu kama hawa walitakiwa wawaambie Serikali ni wapi wamejikwaa na jinsi ya kurekebisha lakini inavyoonekana ni kutafuta mbinu za kulazimisha kufikia malengo ya kodi yaliyowekwa. Hawa wanaanza kudai ni watu wachache wanalipa kodi, na wengine ni kuibuka na maeneo mapya kabisa ya kodi kulazimisha watu walipe.
Serikali itafakari vizuri kama kodi zimepungua wabaini sababu na kuzifanyia kazi na sio kulazimisha kukamua kodi kwa nguvu maana kufanya hivyo wataathiri mzunguko wa fedha zaidi kwenye jamii.
Ni kwa bahati mbaya TRA wao ni wataalamu wa kukusanya kodi, wao wanachotazama ni kuongeza kiwango walichokusanya.
ni vema serikali iwe na taasisi inayoangalia uchumi kwa pamoja na sio kufikiri kukamua kodi tu bila kutizama watu wanapata nini na kwa njia zipi.