ruby garnet
JF-Expert Member
- Apr 10, 2017
- 2,869
- 3,851
Habari wana JF,
Usiwe na wasiwasi kosa lolote ni kipato kwako.
1. 0 hadi miaka 20
Kuwa mwanafunzi mzuri shuleni na kama utakukuwa unafanya ujasiriamali jitahidi kujifunza uzoefu kidogokidogo na mbinu zake.
2. 20 hadi 30
Tafuta mtu wa kujifunza kwake usitafute makampuni makubwa kwani haya huwa mazuri kwa kujifunza kuchakata(processing) mfano HR wa makampuni makubwa au taasisi kubwa kama Voda, Airtel, hawezi kujua mambo ya masoko yeye atabaki rasilimali watu tu na Mkemia kwenye kiwanda cha mafuta atajua kuchanganya mafuta tu na hatajua mambo ya HR na masoko hii itamunyima fursa ya kujifunza ujasiriamali na hivyo utakuwa kama sehemu ya machine kubwa na wewe hautakuwa machine kamwe lakini ukienda viwanda vidogovidogo vya biashara ndogondogo hapa utajifunza mambo mengi sana kwani wewe unaweza kuwa meneja, HR, Afisa Masoko kwa wakati mmoja etc. Hii itakupa uwezo wa kujifunza mambo mengi kwa mda mfupi na utaelewa A to Z na hapa utajifunza ndoto(dreams) na uvumilivu wa ujasiriamali hivyo utakuwa machine kamili na siyo sehemu ya machine tu. Hapa siyo umeenda kwenye kampuni gani bali unamfata Boss gani kwani Boss mzuri atakufunza vitu vingi na vizuri tofautitofauti na hivyo utakuwa unapikwa na katika kipindi hiki jitahidi kufanya makosa mengi ya kutosha na ndiyo yatakujenga.
3. 30 to 40
Fikri vizuri na fanya kazi ya kwako binafisi kama kweli unataka kuwa mjasiriamali na hii inaamanisha huu siyo muda wa kutafuta kazi. Weka mbali vyeti vyako hapa elimu yako inatakiwa iwe kichwani na siyo kwenye certificate. Kuna watu wanachekesha sana yaani wakati huu unakuta yupo kwenye ajira harafu anaanzisha ufugaji wa kuku halafu akifukuzwa kazi hata pesa ya kununulia magazeti ya kusoma matangazo ya kazi hawezi kupata kutoka kwenye kamradi kake ka kuku hako na wengine wapo kazini ndiyo wanajisomea miradi ya kwenye facebook na whatssapp harafu wanaanza kuifanyia kazi, huwa na washangaa sana na wengi wao mwisho wao huwa mbaya sana kwani huwa wanatengeneza mifereji ya kupoteza au kutumia mishara yao bure bila la maana.
4. 40 to 50
LIFE START AT 40 MZEEE.
Fanya mambo ambayo upo vizuri nayo usijaribu kuwa unabadilisha miradi kutoka moja hadi nyingine usiyokuwa nayo uzoefu, unaweza ukafanikiwa lakini mlango wa kufanikiwa ni kidogo sana hivyo unapaswa kutazama mambo uliyo fuzu vizuri huko awali.(focus in things your good at it) mjasiriamali hapa anapaswa kuwa vizuri kweli kweli na siyo kuwa na vimiladi visivyo na vinchwa wala miguu.
5. 50 to 60
Wekeza kwa vijana kwa sababu ndiyo watakuwa vizuri kuliko wewe, wategemee waendeshe miradi wao na hakikisha umewapika kwerikweri na wapo vizuri.
6. 60 .........
Tumia muda wako kwa kujibuludisha nenda beach and enjoy yourself. its too late to make the changes.
"Hahahahahahahah wastaafu ndiyo wanaingia na fujo na mbwembwe katika ujasiriamali katika kipindi hiki sijui ujana wao walikuwa wapi?".
Je wewe uko wapi sasa? Tafadhali jipime.