Simchezo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 453
- 365
Wadau, nimekuwa najiuliza sababu hasa ya kuondoa mikutano ya EAC ambayo
Miaka yote imekuwa ikifanyika jijini Arusha. Arusha imepewa heshima na nchi wanachama kuwa na kujengwa makao makuu ya jumuia hii, leo hii serikali yetu haitambui heshima hiyo tuliyopewa kwa kufanya mikutano hii mikubwa na muhimu Ikulu Dar es Salaam. Arusha ina historia ndefu sana ya ku host mikutano mikubwa tangu enzi za Baba wa Taifa, zipo kumbi na hoteli za kimataifa. Pia Arusha ipo karibu na vivutio vyetu maarufu duniani kama Serengeti, Ngorongoro na Kilimanjaro. Mikutano ikifanyika Ars ni rahisi kwa wageni wengi kutembelea vivutio vyetu kabla ya kuondoka badala ya kuwafungia Ikulu Dar. Nalifikiri hili likifanyika litawapa moyo marais kuhudhuria badala ya kutuma wawakilishi kama ilivyofanyika juzi ambapo rais pekee aliyehudhuria ni Museveni.