Nakubaliana na wewe kabisa mkuu, tatizo tunztofautiana sana, sio kila mtu ni mzuri kwenye biashara. Kuna mtu akipewaa 15M leo ukija ndani ya miezi 6 huenda ukamkuta hana hata senti, na kuna mwingine mpe 1M tu ndani ya mwaka hautaamini anavyoizungusha.
Sasa kwa kua vipato vinatofautiana na hatuwezi kufanya biashara, kuna watu ni afadhali kile kidogo wanachokipata wakielekeze kwenye kitu cha maana japo ujenzi wa aina hii unakua wa kusuasua sana kutokana na ufinyu wa bajeti.
Hoja yako ya kukopa ili uzalishe ina mashiko kama unauwezo, uzoefu na fursa za biashara zipo.