Mikataba ya Madini...tujikumbushe baadhi ya misimamo ya serikali iliyowahi kutolewa bungeni!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,267
23,203
Desemba 5, 2008...

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, amesema mikataba ya uchumi na kibiashara inayosainiwa nchini, haiwezi kuwekwa wazi kutokana na ushindani wa kibiashara.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wandishi wa habari kuhusu usiri uliopo katika utiaji saini wa mikataba ya madini ambayo katika siku za hivi karibuni imekuwa ikipigiwa kelele za kutoifaidisha nchi.

Alisema kamwe mikataba hiyo haiwezi kuwa wazi wakati wa mchakato na utiaji saini lakini itawekwa wazi katika utekelezaji tu baada ya makubaliano hayo kuafikiwa.

"Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi na hata baadhi ya viongozi wakihoji usiri wa nini na kwa faida ya nani? Ukweli ni kwamba huwezi kuweka wazi mkataba na mwekezaji katika hatua za awali kwani huwezi kujua nani atakuja na wazo kama la yule wa awali, kwa hiyo ni ushindani wa kibiashara na si vinginevyo, kitakachowekwa wazi ni utekelezaji, kwa wabunge na wananchi kwa ujumla," alisema Malima.

Alisema katika biashara kuna watu husikiliza nani anataka kufanya nini, kwa hiyo kuwekwa wazi kwa mikataba hiyo kunaweza kuathiri nchi kukosa wawekezaji kutokana na mwekezaji mwingine kuchukua siri au wazo la mwenzake na kumzunguka.

"Kinachofanyika kabla ya kusaini mkataba wewe kama mwekezaji ni kupata maelezo yako, kwamba utafanya hili na lile, utalipaje kodi, na vitu kama hivyo, kwa hiyo kujianika kwako hadharani (mwekezaji), ni kumuwezesha mwenzako kutaka kufanya ulichokusudia, hakuna mazingira ya rushwa wala kuuza nchi katika suala la kusaini mikataba," alisema Malima.

Moja ya mikataba ya siri iliyowahi kufanywa ni ule wa mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya Barrick ya Uingereza, uliosainiwa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, aliyejiuzulu Februari mwaka huu, Nazir Karamagi.

NB: Tutaendelea kufukunyua maktaba kuzidi kupata msimamo wa serikali ya CCM kuhusu mikataba kwa nyakati tofauti. Wakati huo Rais wetu wa sasa John Pombe Magufuli alikuwa ni Waziri katika serikali ya Kikwete.

Baada ya kuapishwa mwaka 2015, hii illikuwa ahadi ya Rais Magufuli kwa viongozi wastaafu...

"Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wewe pumzika kwa raha zako , upo salama watachonga wee lakini mimi kama Rais wa awamu ya tano nipo tayari kuwalinda watumishi wote wastaafu kwa kuthamini mchango wao ndani ya taifa hili," aliahidi Rais Magufuli.

Na juzi kamteua mkewe Kikwete, Salma, kuwa Mbunge...!
 
Magufuli ajue kwamba one man show haimpeleki popote.
Tatizo la Tanzania ni la kimfumo na limesababishwa na kuwa na katiba ya hovyo..
Magufuli akitaka kushinda hii vita, aweke mfumo imara uliosimikwa kikatiba, tena ile ya warioba.
Sitashangaa hii vita akiwa peke yake. Wengine wapo kimwili ila kiroho wanajua nchi inaingia chaka.
Mfumo ndo utakaopambana, na sio yeye peke ake..
 
Magufuli ajue kwamba one man show haimpeleki popote.
Tatizo la Tanzania ni la kimfumo na limesababishwa na kuwa na katiba ya hovyo..
Magufuli akitaka kushinda hii vita, aweke mfumo imara uliosimikwa kikatiba, tena ile ya warioba.
Sitashangaa hii vita akiwa peke yake. Wengine wapo kimwili ila kiroho wanajua nchi inaingia chaka.
Mfumo ndo utakaopambana, na sio yeye peke ake..
Huyu malima si juzi tu alitaka kutolewa roho??
 
Our enemies are innovative and resourceful, and so are we. They never stop thinking about new ways to harm our country and our people, and neither do we....G.W.Bush
 
Back
Top Bottom