kwa mara ya kwanza tulitaka kuexperience usafiri wa majini kupitia kipumbwi
sikua najua usafiri wa huko ni wamajahazi, walikua wanatumia msamiati wa neno "chombo" mimi nikijua ni aina flani ya meli nabhata skujisumbua kujua chombo ni kipi
safari haikua mbaya had kufikia pangani kizaazaa kikaanza kuvuka pale na pantoni ikalala upande tulokua tumekaa wee nilipiga kelele naona watu wote waanitolea macho, mimi hapo ni yarabi tusitiri tuvuke, Allah akbar, subhanallah, astaghfirllah yan nilileta dhakari ambazo sijawah kufanya tangu nazaliwa tulifika kwa mbinde yan ile pantoni ilikua inavutana na maji naupepo
tukaelekea kipumbwi tulifika kama saa kumi jioni hoi hapo tukaulizia usafiri, nauli na taratibu zingine. Kweli tukalipa nauli pale kusubiri safar kuulizia hilo jahaz linaondoka saa tisa alfajiri kuelekea zenji - Mkokotoni, tukajiambia na mama hapa tutanyooka na njaa wasafiri wenzetu wakaanzisha utaratibu wa kuchangisha hela za kujipikilisha palepale kweli tukapika ugali wetu na kachumbari samaki ni kama wote yan bei chee nilikula ugali kwa uchu wa samaki tukalala nje na mizigo yetu yan kwa mara ya kwanza nalala nje kwenye mkeka ilipofika mda tukaamshwa haya amkeni wasafiri muda umewadia tukaamka kwenda baharini hammadi nafika nakuta mpaka kulifikia hilo jahaz mnafaulishwa na vijimashua vijidogo dogo sisi tulikua abiria wa mwisho kufaulishwa nakumbuka kitendo cha kuingia kwenye jahaz nilining'inia miguu iko chini mikono imeshikilia jahazi, dude lenyewe lilikua refu nikavutwa hapo nishachanganywa akili,nawaza hiki ndio chombo?? jamani tunakufa leo! najuta mimi nimekifata kifo bila kujua, yan majuto nafs inaniuma safa ilianza nilioga maji s kawaida, nililoa mno halaf tulifika huko katikati majini lile jahaz lilikua sawasawa na maji means kina ni kirefu nikiangalia mbele naona wingu limeshikana na maji pembeni hivohivo tulikotoka hamna hata kibanda ni maji kotekote sitakaa nikasahau mpaka nakufa wallah ,nilitapika mpaka niliishiwa nguvu kibaya zaidi mkitapika mnapewa huduma ya mifuko ukimaliza unaurusha baharini huko,
tulifika salama lakini nilimwambia mama kama usafiri wa kurudi ni huu utarudi mwenyewe mimi utaniacha unguja
salute sana wavuvi, mnarisk sana maisha yenu, bahari inatisha mno mno mimi mpaka leo hata nikipanda meli tukifika mkondoni lazima nilegee sembuse wewe unaezamia kuna mtu aliangusha mshipi alikua mzoefu tu et akashuka kuufata ikawa fatiha madaraka, alikutwa mikokoni amefariki.