Mods
Sasa kufuatia kanuni na taratibu zilizowekwa hapa,
Ndugu yetu Mwigulu Nchemba amevunja kanuni ya sita (6) kutokana na tuhuma zisizo na ushahidi kwa lengo kumdharirisha Mh Dr Slaa na Chama chake katika thread ile isemayo "Red Brigade ni kikundi cha mauaji, wamwagia sumu na nchi kutotawalika",
Lakini Mods mmeendelea kuiacha thread ile wala Mwigulu hajachuliwa hatua zozote,
Je kwa mtazamo wenu mnaona Mwigulu Nchemba hajavunja sheria za jf ambazo aliziridhia kabla ya kujiunga?
Kama hajavunja kipengele hicho basi naombeni ufafanuzi!