mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,172
- 1,074
Yanayoendelea katika siasa za Tanganyika na Zanzibar yana ukakasi mkubwa kumung'unywa kihistoria.
Wananchi wa nchi zetu wana historia ndefu sana juu ya asili zao,malimbuko yao,machimbuko yao na koo zao.
Lakini pia ni hatari sana harakati za matamanio na kiu za kisiasa kuwa chazo za kubaguana,kunyanyasana,kunyanyapaliana,kuhujumiana,kutesana,kuchukiana na kuchukiana kwa kiwango cha kuwa tayari kuuana sababu ya dhamana za vyeo vya kisiasa .
Tunapaswa kujifunza sana toka kwa mataifa yalioendelea na yanayoendelea kiuchumi,kisiasa na kijamii.Maslahi endelevu ya taifa na wananchi kwa ujumla yapaswa kuwa chachu na kipaumbele yakinifu kwa wenye kiu za madaraka kisiasa,kiuchumi na kijamii.