MAPATO YA SERIKALI KUTOKA MIGODI YA DHAHABU YAONGEZEKA: Timu ya Muhongo iliongeza mapato ya Serikali kama ifuatavyo: (1) Migodi inalipa30% CorporateTax. Majadiliano yanaendelea kwa migodi ambayo bado haijaanza kulipa kodi hii. (2) Mrabaha (Royalty) imepandishwa kutoka 3% hadi 4% - migodi yote inalipa (3) Service Levy (inalipwa) kwa HalmashaurI sasa ni 0.3% ya mapato yote ya mgodi Baadhi ya Halmashauri kupata zaidi ya USD 1M badala ya Dola Laki 2/mwaka.

Serikali imeanza kupokea viwango vipya vya kodi kutoka kwa Kampuni za uchimbaji madini hapa nchini, hatua ambayo ni utekelezaji wa makubaliano ya uboreshaji wa viwango vya ulipaji wa mirahaba, kodi ya huduma na ile inayolipwa na makampuni makubwa. Taarifa za uhakika zilizolifikia Dira ya Mtanzania kutoka vyanzo vyake vilivyoko serikalini zimeeleza kuwa kampuni zinazojihusisha na uchimbaji madini hapa nchini zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ikiwa ni utekelezaji wa agizo lilitolewa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kampuni hizo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kampuni hizo sasa zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ya asilimia 30 ya mapato yanayokusanywa na wazalishaji inayolipwa na makampuni makubwa. Kwamba baadhi ya kampuni ambazo hazijaanza utekelezaji wa ulipaji wa viwango vipya vya kodi hiyo ziko kwenye hatua za mwisho za majadiliano na Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo.>>>>>>>>>>> (CHANZO; GAZETI LA DIRA)
Kwahiyo mda wote walikuwa hawalipi,mmeona mdamuafaka wao kulipa ni sasa tena 0.3.laita serikali ingekuwa inakomalia migodi kulipa kodi,Kama inavyokomalia wafanyabiashara wadogowadogo,basi nchi hii isingehitaji Misada toka nje
Serikali imeanza kupokea viwango vipya vya kodi kutoka kwa Kampuni za uchimbaji madini hapa nchini, hatua ambayo ni utekelezaji wa makubaliano ya uboreshaji wa viwango vya ulipaji wa mirahaba, kodi ya huduma na ile inayolipwa na makampuni makubwa. Taarifa za uhakika zilizolifikia Dira ya Mtanzania kutoka vyanzo vyake vilivyoko serikalini zimeeleza kuwa kampuni zinazojihusisha na uchimbaji madini hapa nchini zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ikiwa ni utekelezaji wa agizo lilitolewa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kampuni hizo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, kampuni hizo sasa zimeanza kulipa viwango vipya vya kodi ya asilimia 30 ya mapato yanayokusanywa na wazalishaji inayolipwa na makampuni makubwa. Kwamba baadhi ya kampuni ambazo hazijaanza utekelezaji wa ulipaji wa viwango vipya vya kodi hiyo ziko kwenye hatua za mwisho za majadiliano na Wizara ya Nishati na Madini kuhusu suala hilo.>>>>>>>>>>> (CHANZO; GAZETI LA DIRA)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAMIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
TANGAZO.
Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014.
Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.
Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015

hivi huwa mnasomaga habari kweli kabla ya kuchangia? au huwa mnakurupukaga tu?ni habari njema hii hongera sana Waziri Simbachawene na timu yako
30% ni sheria, wala sio agizo!