Migodi hatarini kufungwa kufuatia agizo la Rais Magufuli

mambucha

JF-Expert Member
Sep 23, 2013
279
160
Migodi ya Bulyanhukulu na Buzwagi hatarini kufungwa kutokana na agizo la Rais Magufuli.

FB_IMG_1488606600498.jpg
 
Naangalia naona akili za watanzania zilivodumaaa jana share za acacia ktk stock markt zimeshuka kwa 18℅ sasa angalia impact kwenye export mapato, kodi za ndani, employment zote zitakula kwa watanzania dah kuna mtihani mkubwa unakuja
 
Migodi ikifungwa serekale itajiharishia! Hivi si huwa nasikiaga kuna watu wa kusimamia upimaji wa madini kote huko? Sasa nini kimeshindikana kuhakikisha kule wanakoenda kuyeyushia tunakuwa na watu wetu?
 
kwa kuweka sawa tu, hawa watu waliingia mkataba wa kuchimba dhahabu pekee, ambapo serikali inakata kodi, lakini hizi wanaiita masalia by products(concentrates) hizi hazipo kwenye mikataba inawezekana kabisa zilikuwa hazikatwi kodi,

concentrates/by product masalia, huu ni muunganiko wa madini yenye ukaribu sana kwenye periodict table, kama SILVER,GOLD,COPPER NK.
haya yote yanapatikana kwenye sulphate ores, ambayo kwa teknolojia ya kawaida wanayotumia hawawezi kutenganisha..

lakini hili ukiangalia wamefanya hivi kwa makusudi tu kama tukiwazuia watatafuta njia mubadala tekinolojia ya uchenjuaji inakua kila siku..

kama wakiona vipi waende tu lakini najua ndo mwanzo wa kuja na njia mpya au kurudi mezani tena.
 
Lazima ajira ya kusafisha mchanga na kupata dhahabu ibaki kwetu.

Hayo makampuni sasa yataacha "kupata hasara" kwa kuacha kusafirisha mchanga na badala yake yasafirishe dhahabu.

Hii ni awamu ya serikali inayotumia akili. Enzi za mikataba ya Kafumu ya kuruhusu madudu kama kuuza mchanga wa dhahabu badala ya dhahabu yenyewe zimekwisha.

Viva Magufuli. Let us do the right thing at any cost.
 
Migodi ikifungwa serekale itajiharishia! Hivi si huwa nasikiaga kuna watu wa kusimamia upimaji wa madini kote huko? Sasa nini kimeshindikana kuhakikisha kule wanakoenda kuyeyushia tunakuwa na watu wetu?
Good point.Na kusema kweli mining Industry imedorora sana kwa sasa Tanzania investors wanapita zao haooooo West Africa
 
Tisha toto hiyo.mchanga ni substance ya mwisho kabisa baada ya kupata dhahabu,wala haupo kwenye extraction process ya mdhahabu.Ila ili kuongeza faida nao mchanga unachekechwa unatoa mabaki amabayo wanayauza juu kwa juu.Sasa wafunge mgodi kwa kukosa kuuza mabaki tena juu kwa juu hata serikali haiambiwi kilichopatikana na bei yake.
Wawekezaji waliozoea kufanya Tanzania shamba la bibi,inabidi wabadilike tu,nchi imeshikwa na mtu makini sana
 
Back
Top Bottom