Miezi 6 ya tathmini isiwe kwa rais pekee

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Nadhani sasa hebu tuache kulalama na tumsaidie rais kufanya kazi.
Kila mtu atoe tathmini ya miezi hii sita amefanya nini kilichokuwa tofauti au chenye tija zaidi ambacho anadhani kina tija kwa nchi yetu.

Unajua ni rahisi sana kumlaumu rais kuliko kutenda wewe mwenyewe! Tunaweza kudhania kuwa kwa kulaumu ndio tunamkumbusha rais kuwa sisi ndio waajiri wake, lakini kwa maana nyingine tunampa haki rais aendelee kuamini kuwa nchi hii ni yake na yeye ana haki zaidi, ndio maana vitu vikiwa hovyo wote tunamlaumu yeye.

Kwa ukweli huo kila mtu angependa alinde kazi zake na awe mkali na aongoze kila jambo!Kama kila mtu angekuwa anatimiza wajibu wake, kwa wenye taaluma zao wakakubali wajibu wao bila ya visingizio na wangeshiriki kufanya yaliyo wajibu, kugundua mbinu mpya na bora zaidi zenye kujenga na penye changamoto tungeacha longolongo na kukubali kuwajibika, then rais angekuwa hana haja ya kuwa kama kiranja/Mwalimu wa zamu.

Tubadilike!

Note: Hakuna jambo jipya zaidi katika ofisi yangu ndani ya muda tajwa, ila muda wa kazi tumeustretch kidogo, beyond Tisa na nusu, na ninatoa huduma kwa watu wengi zaidi.Nahisi nimeweza kuongeza tija kidogo!Wewe je?
 
Hahahahaah Walisena jamaa anataka one man show ndio maana yule Mama kanyimwa hata Mikasi this time...
 
Ni wakati wao wa kustand out from the cloud!

Lukuvi, Mwigulu, Makonda wote wanafanya kazi, hakuna anayewazuia wala anayewalazimisha kama walivyo mawaziri wengine!

Watu wanapenda kutoa visingizio Ila kwa kweli hatuwajibiki!
 
Kwani wakati anaomba kura si alikuwa anasema kila mara "serikali ya Magufuli"!

Basi hata wenye kukosoa si mbaya vile mashutumu yao wakiyaelekeza kwake
 
Yeye ndo kichwa cha nchi. Wakiboronga mawaziri wake automatically ameboronga yeye.
 
Raisi huyu kazi tunayo. Nangoja amendment ya kwenye katiba ajitangaze raisi wa maisha.
 
Mawaziri wamefungiwa kwenye chupa.....hatujui wanafanya nini na wana vipaji gani.....labda lukuvi
Wafunguke kama sio wanafiki, kama Lukuvi anapiga kazi na wao wajitoe mhanga kufanya kazi bila kuingiliwa na wakiiingiliwa katika majukumu yao wafunguke na ikibidi wajivue kabisa ili tuone
 
Back
Top Bottom