ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,604


Dege la kwanza la Marekani maalumu kwa usafirishaji wa mizigo ya kijeshi lawasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben-Gurion nchini Israel likiwa limebeba mamia ya tani za mizigo yakiwemo magari na vifaa vingine maalum kabisa kwa ajili ya ziara ya Rais wa Marekani, Donald Trump.

Madege mengine 30 kama hayo yanatarajiwa kuwasili nchini Israel yakiwa na magari,magari ya Rais(The beast) na malori ambayo yatakua yamebeba vifaa maalumu(armoured glass) ambayo vitafungwa kwenye madirisha ya hoteli atakayolala Rais Trump.

Ziara hiyo ya Rais wa Marekani itajumuisha watu takribani 900: wafanyakazi wa kuendesha hvyo vifaa, wahudumu wa afya, wanausalama, wataalam wa kompyuta, waratibu wa ziara na maafisa wa ikulu.


Maafisa 20 wa secret service ndio watakaoandamana na Rais na ndio watahusika na usalama wake.
Baadhi ya maafisa wa ngazi mbalimbali wameshawasili ili kushirikiana na maafisa wenyeji wa Israel kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwa maeneo yote ambayo Rais Donald Trump anatarajiwa kutembelea: Jerusalem, Bethlehem, Masada na Ramallah.