ANDENDEKISYE C
Member
- Mar 5, 2012
- 90
- 23
MIDAHALO YA WAGOMBEA UBUNGE- NDANI YA VYAMA-CHADEMA IONYESHE NJIA.
Utangulizi.
Nimeshiriki chaguzi nyingi sana maishani mwangu. Na mwaka huu nimeweka wazi dhamira yangu ya kushiriki tena. Katika kushiriki kwangu, nimeona mapungufu ktk vyama husika inapokuja kura za maoni. Kwa mfano mwaka huu,ndani ya CHADEMA- jimbo la Rungwe Magharibi, Mkoani Mbeya, lina watu walioandika barua za kugombea Ubunge wapatao 18-na wataongezeka zaidi. Jimbo la Segerea kuna wagombea 11 kwa taarifa nilizonazo. Hali ni hivyo nchi nzima…Hali ni tofauti na miaka ya nyuma wakati unakuta pengine jimbo zima mgombea ni mmoja ama wawili tu.
Ni wakati muafaka sasa chama chetu kibadili mbinu ya kuchambua wagombea. Huko nyuma, kwenye chaguzi zote, unakuta watu wanapewa pengine dakika 5 mpaka 10 kujieleza, na maswali matatu yanaulizwa. Kwa mgombea ubunge kujieleza kwa muda huo si sawa kabisa, ukichukulia ukweli kwamba kuna wapiga kura wanakuwa pengine hawajamfahamu vizuri mgombea.
Tukumbuka tunatafuta mtu wa kuwakilisha jimbo. Ni nafasi kubwa na muhimu sana. Tumeona namna ambavyo wabunge wazuri wanasaidia kubadilisha nchi, majimbo na maisha ya watanzania, na kwa wale wabunge mizigo tumeona ambavyo wanaligharimu taifa.
Kuna umuhimu wa jambo hili- CHADEMA kwa kuwa mwaka huu wagombea ni wengi sana- iangize majimbo yote kuwepo kwa midahalo ya wazi ya wagombea wake kujieleza je wao ni nani? Wamefanya nini ndani ya chama na nje ya chama kisiasa? Je wamefanya nini kusaidia jamii mpaka wakati huu nje ya siasa, je, wanaulewa kiasi gani nambo ya majimbo yao, nchi na dunia-hili likichagizwa na kiwango chao cha elimu, na pia mbali na Ilani ya chama, je wamejipangaje kuleta mabadiliko chanya ktk majimbo yao, mikoa yao, nchi na dunia.
MIDAHALO ITATUSAIDIA KUCHAMBUA WALE KWELI WANAOSTAHILI KUKABIDHIWA BENDERA ZA CHAMA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU….Na watakaogopa basi tujue wazi kwamba hawafai.
Si vibaya vyama vingine vikaiga huko mbele ya safari.
Maoni yanakaribishwa