palikuwepo mchezo ambao unachora chini vyumba vyumba halafu unarusha kipande cha kigae na kisha unakisukuma kwa mguu toka chumba kimoja hadi kingine. Halafu unatembea katika hivyo vyumba huku umefumba macho na kila hatua moja unauliza wenzako "Am I right?" ingawa kwakweli tulikuwa tukisema "Marait?". Ulikuwa ni mchezo unaompa mtoto changamoto na pia ni mazoezi mazuri sana. Sijawahi kuuona sasa miaka mingi kabisa.
Kilimanjaro tuliuita au tikri. Nimchezo nilio umudu sana kuliko mingine nliwekwa wa mwisho kira mara sababu nliweza kucheza bila kukosa mpaka mwisho. Nlifinywa sana na mama mpaka nlimchukia kisa michezo. Watoto wa sasa zzzzro kabisa. Wanajua wasap,twta,facebook. Basi daah shule ubunifu ushindani ujanja hakuna kituMwanza unaitwa Dama sijui maeneo mengine wanauitaje,baadhi yakanuni kigae kikikaa mstarini umebau(kushindwa)au ukikanyaga mstari,pia kunamuda unatakiwa kuweka kigae mguu moja huku mwingine ukitumika kuruka vyumba...nice tulienjoy sana kipindi hicho