Michezo ya wanasiasa wetu na hatma ya Taifa letu

Ex Spy

JF-Expert Member
Jan 15, 2007
222
1,826
Assumption: We are democratic!

You will solve it yourself.

Siasa za Tanzania:

Kuna chama kinatawala, baadhi ya wanachama hata walio na vyeo vya juu hawajui who is who ndani ya chama maana maamuzi mengine wanalazimishwa kuyatekeleza. I know this, I have been with these bunch of loosers.

Kuna wapinzani, hawa pia wa ajabu kiasi chake. Maamuzi yao yanatokana na wale wanaoendesha chama kinachotawala. Ajabu pia, huku kwenye vyama tunaita pinzani kuna watu wana nafasi (wengine ni wabunge) hawajui namna gani vyama vyao vinaendeshwa. Hawajui mchezo unachezwa na nani (the game players).

Pande zote mbili zina vyanzo vya fedha visivyowekwa wazi kwa wananchi na kamwe ukweli hautaelezwa kwakuwa wanaojua ukweli huo ni sehemu ya syndicate.

Wanaocheza mchezo:
Hawa nao wanashangaza kidogo, hukutana na hawa wanaoigiza kuongoza vyama vya siasa na kupanga igizo liende episode gani na washiriki wawe kina nani. Kwa kiwango kikubwa hufanikiwa lakini 2014 na 2015 walichanganyikiwa kidogo baada ya mchezo kukosewa script; bahati fixer akafanya kazi yake.

Kundi hili lina walau watu 3 katika makao makuu ya kila chama na watu hawa hufanya kazi kwa umakini mkubwa.

Wafanyabiashara:
Wakati wengine wakidhani ni wafanyabiashara huru lakini nao ni sehemu ya kundi kuu ya wachezeshaji mchezo.

Swali kwa wachezaji hawa: Kwanini huwa mnakutana mida ya usiku mkubwa sana na nini sababu ya kukutana baharini na 'VIP Clubs'?

Wanaotumika:
Hawa wengine hata hawajui kama wanatumika, hujitahidi sana kufanya kazi ya wanaowatuma. Wengine hata hawaujui mchezo, wengine wanalipwa ili wacheze mchezo huu.

Huenda ndivyo inatakiwa mchezo huu wa Siasa ufanyike na huenda utaratibu huu una faida lakini una future na ukuaji huu wa teknolojia?

Mtaendelea kuwapoteza wanaoushtukia mchezo huu hadi lini?
 
Ndio maana wengine tumeacha ushabiki wa vyama... Tunapima kila hoja kwa jicho la tatu... Kuna issues ukizifikiria sana utajua kuna "nguvu" inayoendesha siasa zetu ...kama huna maslahi ya moja kwa moja na hivi vyama vyetu ..lazima ubaki na maswali mengi...
 
Assumption: We are democratic!

You will solve it yourself.

Siasa za Tanzania:

Kuna chama kinatawala, baadhi ya wanachama hata walio na vyeo vya juu hawajui who is who ndani ya chama maana maamuzi mengine wanalazimishwa kuyatekeleza. I know this, I have been with these bunch of loosers.

Kuna wapinzani, hawa pia wa ajabu kiasi chake. Maamuzi yao yanatokana na wale wanaondesha chama kinachotawala. Ajabu pia, huku kwenye vyama tunaita pinzani kuna watu wana nafasi (wengine ni wabunge) hawajui namna gani vyama vyao vinaendeshwa. Hawajui mchezo unachezwa na nani (the game players).

Pande zote mbili zina vyanzo vya fedha visivyowekwa wazi kwa wananchi na kamwe ukweli hautaelezwa kwakuwa wanaojua ukweli huo ni sehemu ya syndicate.

Wanaocheza mchezo:
Hawa nao wanashangaza kidogo, hukutana na hawa wanaoigiza kuongoza vyama vya siasa na kupanga igizo liende episode gani na washiriki wawe kina nani. Kwa kiwango kikubwa hufanikiwa lakini 2014 na 2015 walichanganyikiwa kidogo baada ya mchezo kukosewa script; bahati fixer akafanya kazi yake.

Kundi hili lina walau watu 3 katika makao makuu ya kila chama na watu hawa hufanya kazi kwa umakini mkubwa.

Wafanyabiashara:
Wakati wengine wakidhani ni wafanyabiashara huru lakini nao ni sehemu ya kundi kuu ya wachezeshaji mchezo.

Swali kwa wachezaji hawa: Kwanini huwa mnakutana mida ya usiku mkubwa sana na nini sababu ya kukutana baharini na 'VIP Clubs'?

Wanaotumika:
Hawa wengine hata hawajui kama wanatumika, hujitahidi sana kufanya kazi ya wanaowatuma. Wengine hata hawaujui mchezo, wengine wanalipwa ili wacheze mchezo huu.

Huenda ndivyo inatakiwa mchezo huu wa Siasa ufanyike na huenda utaratibu huu una faida lakini una future na ukuaji huu wa teknolojia?

Mtaendelea kuwapoteza wanaoushtukia mchezo huu hadi lini?

Mim nimeelewa tu. Hapo baharin. Nikakumbuka bahari bichi mission na mshenga
 
Uelewa mdogo sana wa WaTz. Kwani ushindi unaopatikana hapa kwetu huko mnako refer km wakomavu haupstikani?
 
Kumbe hili la lowasa .mbowe na rostam kukutana mida ya usiku sana linajulikana
 
Mkuu naona unamsema mzee wa fursa January makamba kijanja, maana wenzake ndiyo wanasema hukutaka na wafanyabiashara wanaotaka vibali vya sukari Usiku wa manane.
 
Ndio maana wengine tumeacha ushabiki wa vyama... Tunapima kila hoja kwa jicho la tatu... Kuna issues ukizifikiria sana utajua kuna "nguvu" inayoendesha siasa zetu ...kama huna maslahi ya moja kwa moja na hivi vyama vyetu ..lazima ubaki na maswali mengi...
Jamaa anampelekea January msg kijanja tu wala si zaidi chunguza kwa makini utabaini Ukweli.
 
Wanaotumika:
Hawa wengine hata hawajui kama wanatumika, hujitahidi sana kufanya kazi ya wanaowatuma. Wengine hata hawaujui mchezo, wengine wanalipwa ili wacheze mchezo huu
Lizaboni na Simiyu Yetu
 
Wanaotumika:
Hawa wengine hata hawajui kama wanatumika, hujitahidi sana kufanya kazi ya wanaowatuma. Wengine hata hawaujui mchezo, wengine wanalipwa ili wacheze mchezo huu
Lizabon yupo nyumbani kwa Lugumi kajificha maana anatafutwa na kitwanga amrejeshee pesa zake alizomlipa ili amtetee Mitandaoni.
 
Ukisoma hii thread:

Chanzo chetu cha habari ndani ya CHADEMA kimedokeza kuwa kumekuwa na uhamisho mkubwa wa fedha mara tu ruzuku inapoingi kwenye akaunti. Zaidi ya shilingi milioni mia mbili zimekuwa zikihamishwa kila mwezi kwa madai kukijenga chama ila jambo la kustaajabisha ni kuwa pesa hizo huamishiwa kwenye akaunti mpya zilizofunguliwa katika benki moja ya biashara kisha kutolewa taslimu.

----->

Chanzo kingine kilitudokeza kuwa ‘pesa zinazohamishwa baada ya kutolewa benki taslimu ni malipo kwa mwanasiasa mkongwe aliyehama kutoka CCM na Kuja CHADEMA kwa mujibu wa makubaliano’’, ameendelea ndugu yangu mwenyekiti amekuwa ‘mbogo’ hataki kuulizwa kuhusu suala hili na ametamka yeyote atakayeendeleza mjadala atatimuliwa’’.

------>

‘Ndugu yangu sasa hivi mwenyekiti hana maamuzi na baadhi ya viongozi wameshaambiwa wasichukuwe fomu kugombea nyadhifa kwenye uchaguzi ndani ya chama unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018.

‘Ninachokwambia baadhi ya viongozi wapo sababu ni wabunge lakini kulekea uchaguzi mkuu 2020 mtasikia mengi, kuna fukuto kubwa sana na mwenyekiti kwa sasa amefanya shingo ngumu’’

Napata picha kuwa kilichoandikwa kwenye bandiko kuu kuwa kuna informers kwenye vyama ni kweli.

Hii inaashiria nini?
 
Ukisoma hii thread:

Napata picha kuwa kilichoandikwa kwenye bandiko kuu kuwa kuna informers kwenye vyama ni kweli.

Hii inaashiria nini?
inawezekana ikawa ni ukweli lakini kutokana na reputation ya huyu mtoa taarifa kuwa na uchama sana, napata tabu kuziamini
 
Back
Top Bottom