kitalembwa
JF-Expert Member
- Jul 12, 2014
- 7,820
- 20,805
Hua unahudhuria Jumuiya mkuu?Unakuta mtu mlisoma wote, pengine std 7, form 4, au chuo, kitambo mlishapotezana ,anaanza kukutafuta kwa kasi ya 5G, anataka mchango! Msg haziishi , Mara kupigiwa simu!
Unajikuta ghafla new WhatsApp group heading "mchango wa,,,,,,,," Mimi nikiona hivyo huwa naleft haraka Sana, mtu anakamomaa kukucheki manually, namjibu simpo tu sina pesa kwa Sasa! Sitoi ahadi maana itakuwa usumbufu usiokoma!
Harusi michango, send-off michango, kitchen party michango, kipaimara michango, komunio michango, jubilei michango , engagement michango !!!!
Sikatai kuwa dhana ya kufanya sherehe/shughuli ama tafrija Ni kuweka umoja hususani ndugu, marafiki n.k ! Lakini mwenye sherehe akijiona Hana uwezo wa kukidhi hayo kwa Nini asumbue watu wamchangie ?? Nimeshuhudia watu kadhaa wanafilisika ama kuingia katika madeni kwa sababu tu ya kufanya sherehe ili afurahishe watu!
Binafsi hizi habari za michango Sina habari nazo kabisa, huwa natoa jibu la Moja kwa moja Sina pesa! Nachangiaga misiba tu , Tena huwa naangalia sio misiba yote nachanga,,,, unakuta mtu Ni jirani yako, amefiwa na ndugu wa mke wake, anaenda kijijini kuzika, nakupaje mchango ??
Michango ilinifukuzisha mda Sana !!! Huwa naenda kanisani tu,,,! Sadaka na zaka huwa natoa! Inatosha Sana ,Hua unahudhuria Jumuiya mkuu?
Basi una hatari mkuu niulize kwaniniMichango ilinifukuzisha mda Sana !!! Huwa naenda kanisani tu,,,! Sadaka na zaka huwa natoa! Inatosha Sana ,
Bora usije kuniomba huo mchango ili nikose hio heshima ambayo haina lolote mbele za macho ya watu kumbe huku kunanidumaza kimaendeleo !!!Ila kuja kuombwa mchango nako kuna heshima.
Unakutana na mtu ana umri zaidi ya 40 na hajawahi hata kuletewa kadi ya mchango wowote.
Hakika !Hii michango haina tija, mtu ukiwa na jambo kama hili familia ndio inatakiwa kuku support na marafiki watakao wiwa wenyewe bila kushurutishwa
UnaambiwaIla kuja kuombwa mchango nako kuna heshima.
Unakutana na mtu ana umri zaidi ya 40 na hajawahi hata kuletewa kadi ya mchango wowote.
Unafikiri nikifa sitazikwa kwa sababu sishiriki jumuiya? Hio Ni Big No!Basi una hatari mkuu niulize kwanini
Ushajibu tayari mkuuUnafikiri nikifa sitazikwa kwa sababu sishiriki jumuiya? Hio Ni Big No!
Nilikula ban kwa hii sentensi atizame.Nchemba atizame na huku
Ova
Mkuu umeongea point sana..uko kama mimi..yaani mmepotezana miaka mingi tena wakati ule wa kuanza kutafuta maisha hawa watu hawakuwepo wanakuja saa hizi kwa lengo la kusaidiana wakati angalau unajimudu na maisha yako.Unakuta mtu mlisoma wote, pengine std. 7, form 4, au chuo, kitambo mlishapotezana, anaanza kukutafuta kwa kasi ya 5G, anataka mchango! Msg haziishi, mara kupigiwa simu!
Unajikuta ghafla new WhatsApp group heading "mchango wa... ." Mimi nikiona hivyo huwa naleft haraka sana, mtu anakamomaa kukucheki manually, namjibu simpo tu sina pesa kwa sasa! Sitoi ahadi maana itakuwa usumbufu usiokoma!
Harusi michango, send-off michango, kitchen party michango, kipaimara michango, komunio michango, jubilei michango, engagement michango!
Sikatai kuwa dhana ya kufanya sherehe/shughuli ama tafrija ni kuweka umoja hususani ndugu, marafiki n.k Lakini mwenye sherehe akijiona hana uwezo wa kukidhi hayo kwa nini asumbue watu wamchangie? Nimeshuhudia watu kadhaa wanafilisika ama kuingia katika madeni kwa sababu tu ya kufanya sherehe ili afurahishe watu!
Binafsi hizi habari za michango sina habari nazo kabisa, huwa natoa jibu la moja kwa moja, sina pesa! Huwa nachangia misiba tu, tena huwa naangalia, sio misiba yote nachanga. Unakuta mtu ni jirani yako, amefiwa na ndugu wa mke wake, anaenda kijijini kuzika, nakupaje mchango?