Michango imezidi RC

Sure wanataka wenyewe wawe na bima wakati asilimia kubwa ya waumini wao haziwezi kunilipia bima. Na kwenye matumizi yao utasikia milioni 200 zimetumika kununua funiture na kuweka A. C kwenye nyumba za mapadri hakuna ata senti inayorudi kwenye jamii.
 
Shida haipo kwenye kujitoa. Shida ipo kwenye kupangiana kiasi cha kutoa.
 
"Mtu Hutoa Kama Vile Ameazimia Moyoni Mwake”

Badala ya kutaja kiasi hususa cha pesa, Paulo alipendekeza tu kwamba ‘kila mmoja atenge kiasi cha fedha kadiri ya mapato yake’ katika siku ya kwanza ya juma. (1 Wakorintho 16:2) Kwa kupanga na pia kutenga kando kiasi fulani kwa ukawaida, Wakorintho hawangehisi kwamba wanashurutishwa kutoa michango yao, wala hawangeitoa kwa sababu ya msisimuko tu wakati Paulo alipofika. Kila Mkristo angeamua kibinafsi ni kiasi gani angetoa, kulingana na ‘alichokuwa ameazimia moyoni mwake.’—2 Wakorintho 9:5, 7.

Wakorintho walihitaji kupanda kwa wingi ili wavune kwa wingi. Paulo hakusema lolote kuhusu kutoa kupita uwezo wa mtu. ‘Sikusudii iwe vigumu kwenu,’ Paulo akawahakikishia. Michango ‘ilikubalika hasa kulingana na alicho nacho mtu, si kulingana na kile ambacho mtu hana.’ (2 Wakorintho 8:12, 13; 9:6) Katika barua fulani aliyoandika baadaye, mtume alionya: “Ikiwa yeyote hawaandalii kitu . . . wale walio washiriki wa nyumbani mwake, ameikana imani naye ni mbaya zaidi kuliko mtu asiye na imani.” (1 Timotheo 5:8) Paulo hakuwahimiza watu watoe kwa njia iliyovunja kanuni hiyo.

Inafaa kuona kwamba Paulo alisimamia ukusanyaji wa ‘mchango kwa ajili ya watakatifu’ waliokuwa na uhitaji. Maandiko hayasemi popote pale kwamba Paulo au mitume wengine walipanga michango itolewe au walipokea fungu la kumi ili kugharimia huduma zao wenyewe. (Matendo 3:6) Paulo alishukuru daima kwa zawadi ambazo watu walimpelekea, naye alikuwa mwangalifu asiwatwike ndugu zake “mzigo ulemeao wenye gharama.”—1 Wathesalonike 2:9; Wafilipi 4:15-18.
 
Kwani mfano ukienda kusali na kutoka bila kuchanga watakuzuia kwenda tena Jumapili ijayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Utasali tu, tatizo hii michango inadaiwa huku kwenye jumuiya. Nanusipoitoa inamaaana ata huduma za kanisani hutapata maana jumuiya ndo zinatunza hzo kumbukumbu
 
Bima ya mapadre?? kanisa katoliki si lina mahospital dunia nzima? wanahitaji bima ya nini sasa
 
mkuu jaribu kusoma roman empire ndio utaelewa catholic nini hasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeeleza vema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza inabidi ujiulize kama mungu yeye ndio aliumba vitu vyote kwanini mumuchangie hela zote hizo?

Sent from my SM-G950F using Tapatalk
 
Nilijua ni huku niliko mimi tu kumbe kila mahali,yaani kwa hapa nilipo wanakuangalia biashara au kazi uliyonayo then unapangiwa kiasi unachopaswa kutoa,na hiyo inaanzia huku kwenye jumuiya.Wengi wanaacha kusali na wapo wanaohama madhehebu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…