jamaa anahaki Kuwa hapo alipo ukiwaacha Kuwa the best kwenye NBA jamaa ni Smart, Kama Mike Tyson angekuwa Smart naye angekuwa Bilionea! Hongera zake MJ.
Mkuu Pazi, watu wengine wameshaandikiwa tangu mbinguni kama wao ni wa kupata tu, hata wapigwe vita namna gani lakini mambo yao siku zote hunyooka tu, ila mie nilidhani Magic Johnson angekuwa billionaire kabla ya Michael Jordan sidhani naye kama atamaliza hata miaka miwili kabla ya kuingia kwenye hiyo Club. Ni kweli Mkuu kuna wengi walikuwa wanapata ngawira chungu nzima lakini leo hawana kitu. Juzi nimesoma article kuhusu Iverson kwamba anashindwa hata kununua hamburger moja ya McDonald!!!! Article ile imenisikitisha sana. Pesa ni mwanaharamu ukijaaliwa kuipata kama hukutuliza akili basi inaweza ikakukimbia yote.
Allen iverson nilikua namkubali sana,kafilisika hivyo!!!!dah pesa mwanaharamu
Duh umetoka umemuongelea Damon Dash nimetoka sasa hivi Worldstarhiphop kumsikiliza anajitetea kuhusu watu wanaosema yeye ni broke hehe.Kamsome Damon Dash...utashangaa..wakati JAy Z anakaribia kuwa billionaire. Dash kafilisika vibaya
Kamsome Damon Dash...utashangaa..wakati JAy Z anakaribia kuwa billionaire. Dash kafilisika vibaya
Umesema kweli ila Floyd nafikiri anajuwa nini anachofanya haitokuwa rahisi yeye kufilisika kirahisi ila tukija Iverson aliendekeza sana Hood na marafiki sio na alikuwa party anazirusha bila mafanikio mapenzi yake kwa watu aliyatumia vibaya aliipenda Hood yake kwa kuwapa pesa ovyo bila Kuwa na chakuingizia pesa, hajafanya Kama Magic Johnson Kuwa na makampuni au Michael Jordan Huyu MJ kwenye viatu alivisimamia Nike kwa akili ya kuijuwa haki yake sio tu kupewa pesa ale Kama Iverson alivyocheza na Reebok yeye ali tizama mshahara tu.Unajua watu weusi wengi hatuna heshima katika pesa ndio maana tunafilisika...mfano mzuri ni Floyd Mayweather
Kama wiki mbili zilizopita nilikuwa naangalia kipindi cha kuwahusu wachezaji wa American Football ambao waliamua kufunguka kuzungumzia jinsi walivyofilisika. Aisee inasikitisha sana wengi walikuwa wanalia kama watoto. Wengi wao wametoka katika familia ambazo hazikuwa na pesa, basi wanapopata pesa wanajisahau na maisha ya anasa na wakija kutahamaki pesa yote imekimbia na wale waliokuwa wamewazunguka kutafuna pesa zao wote wameingia mitini.
. binadamu huwa tunajisahau mkuu sawa na harusi kitu cha furaha ila wengine watafanya watu wawe na karaha unamlazimisha mtu atoe Laki ya mchango masikini Hana akikwambia Hana unamnunia na harusi humualiki au mtu ukimwambia sina pesa haimaanishi Hana Kabisa Pengine anayo kwa kulipa bili zake na mahitaji Yule aliyenyimwa akiziona umenunuwa kitu ananuna sana wengine wanaroho za kutowa Iverson alikuwa na roho nzuri sana na matatizo yalimfata hajui ayapangilie vipi ushauri wa streets nao unaponza sana wapo ndio wapo sio utakuwa Kama Mc hammer.inasikitisha sana
na the list is so long
hata african footballers wamo
kuna mchezaji NBA kipindi cha lock down ilibidi atafute kazi ya kufagia treni
yaani lock down tu alikuwa chali
inasikitisha sana
na the list is so long
hata african footballers wamo
kuna mchezaji NBA kipindi cha lock down ilibidi atafute kazi ya kufagia treni
yaani lock down tu alikuwa chali