Miaka takriban 40 ya UKIMWI bila Chanjo wala Tiba, kuna tija yoyote ya maadhimisho kila mwaka?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,501
27,000
Salamu ni hapo juu!

Hii kitu sio rahisi kuelewa, what’s the motive behind this?

Kila mwaka tunafanya maadhimisho ya kushangilia 'a world proven failure' kwenye mapambano dhidi ya Virusi Vya UKIMWI! Tunashangilia nini, tena kwa bajeti kubwa na posho kwa washiriki.

Miaka 40, kwenye dunia iliyojaa magwiji kwenye maabara za kitafiti. Haingii akilini kushindwa kabisa, kuna wachache wenye maslahi. Corona hii hapa, miezi kadhaa tu tayari inasemekana chanjo imepatikana. Na pengine ni tiba kabisa, kwanini sio VVU?

Kumekuwa na ripoti mbalimbali za kitafiti zikidai kupatikana kwa chanjo/tiba ya VVU, lakini zimekuwa zikizimwa very soon after!

Je, na hii ya corona itazimwa? Je, kuna nani nyuma ya majanga kama haya ambaye ni mnufaika? Kuna jitihada zozote 'za kweli' zinazoendelea kuondokana na hili janga? Kama zipo, kuna tumaini lolote so far?

Kama hali ndo hii, tunaadhimisha kwa muktadha upi, tunanyoosha mikono na kukiri kushindwa!

Miaka 40, VVU bado vipo na vitakuwepo sana.

PIMA, JITAMBUE, ISHI.
 
Miradi ya Super power country hiyo

UGAIDI .MAGONJWA .SILAHA NA BAADHI YA PEMBEJEO

Ni baadhi ya silahq zinazotumiwa na mataifa makubwa duniani kwaajili ya kujinufaisha kiuchumi na kuteketeza mataifa mengine ambayo wao wanayaona kuwa ni mataifa tishio kwa ustawi wa uchumi wao ..
 
Dawa ipatikane ili wasiendelee kuuzia watu ambao hawajataka kushtuka na kuchukulia vitu poa ! Africa wanaongoza njia ya maambukizi kwa zama hizi ni ngono zembe 99% na watu hawajali!

Dose moja tu ya mwezi ni 300-600$ hii ndio biashara iliyofaidisha mzungu kwa miaka kutokana na ujinga au kuchukulia poa vitu kwa wateja wakuu(Kusini mwa jangwa la Sahara)
 
Dawa ipatikane ili wasiendelee kuuzia watu ambao hawajataka kushtuka na kuchukulia vitu poa ! Africa wanaongoza njia ya maambukizi kwa zama hizi ni ngono zembe 99% na watu hawajali!

Dose moja tu ya mwezi ni 300-600$ hii ndio biashara iliyofaidisha mzungu kwa miaka kutokana na ujinga au kuchukulia poa vitu kwa wateja wakuu(Kusini mwa jangwa la Sahara)

Starehe ya maskini ni pombe na ngono, huo ukanda uliotaja kwanza hata ufahamu tu hawana.... ni kama hawajui kuna UKIMWI.

Achilia mbali malaria, hadi leo hii watu kibao hawajui kujikinga na malaria!!
 
Hulu swala la UKiMWi ni plan yao mabeberu tuu yan miaka 40. Washindwe kupata dawa na chanjo ni uongo tuuu it’s project yao .mbona Covid wamepata chanjo na wamewek jitihada ndan ya muda mfupi
 
Kama kuna mwenye kumbukumbu siku chache kabisa kabla ya Corona ilitangazwa chanjo ya ukimwi UK kwamba seli za wale ambao damu zao hazipati maambukizi ya HIV zilichukuliwa na kupandikizwa wenye maambukizi na baada ya muda virus vilipotea
Sijui ile habari umeishia wapi
 
Back
Top Bottom