Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,915
- 30,259
ZAIDI YA MIAKA 50 ILIYOPITA
Shule ni St. Joseph's Convent School.
Mwaka wa 1967.
Darasa Form 1D.
Class Teacher Mrs. De Souza.
Darasa hili mchanganyiko Wasichana na Wavulana.
Form 1C Wasichana watupu.
Form 1A na Form 1B Wavulana watupu.
Nasoma darasa moja na Edward Makwaia sasa Chief Edward Makwaia wa Siha Usukumani amerithi kiti cha marehemu baba yake Chief David Kidaha Makwaia.
Nimemuona Chief David Makwaia katika runinga taarifa ya habari akiongoza Sherehe ya Wasukuma.
Haraka nimeingia Maktaba nikakuta katika picha zake nyingi nilizonazo hizo nilizoweka hapa ndizo za zamani zaidi mwaka wa 1967.
Picha hizi zimenirudisha nyuma sana.
Katika picha hizo yuko Juma Mwapachu na mdogo wake sasa marehemu Wendo Mwapachu, mama yetu Mary Mackeja akimwangalia Edward akikata keki ya siku yake ya kuzaliwa.
Nyuma ya mama wa kwanza kulia ni Wendo na nyuma ya Edward ni Andrew Gordon.
Mimi wa kwanza kulia nikifuatiwa na William Mfuko na Juma Mwapachu.
Nilipomrushia Ted picha hii kaniandikia, "Sidney tulikuwa wadogo."
Hakika tulikuwa watoto.