Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Ni kama jana tu yaani 5-2-1977, kumbe ni miaka 40 iliyopita.
Muda unakwenda kasi sana, tayari CCM inatimiza miongo minne ya uwepo wake. Baada ya vyama vya ASP na TANU kuunganisha nguvu na kuunda chama kimoja.
Yamefanyika mengi ndani ya uhai wa CCM, mengine mema na mengine mabaya.
Kitu cha muhimu ni kwa CCM kutambua kwamba kuna kipindi mwelekeo wa waliokianzisha ulionekana kupotea. Na kwa sasa kinachofanyika kwa nguvu zote ni kukirudisha chama kwenye mstari sahihi.
Lengo la chama chochote cha siasa ni kuendelea kushika dola kwa kuziuza sera zake kutokana mahitaji ya maisha ya wananchi.
Miaka 40 ya CCM kwa wengine imekuwa ni michungu na kwa wengine imekuwa ni neema. CCM kwa kuweza kuwepo madarakani kwa muda mrefu, kimekuwa ni chama ambacho kinayo hazina kubwa ya watu wenye uwezo wa kukiongoza na kutekeleza ilani mbalimbali za uchaguzi.
Lakini huko tuendako, wale vijana wengi ambao wamezaliwa ndani ya hii miaka 40 ya uhai wa CCM, wanayo mawazo, hisia na vionjo vya aina mbalimbali. Na sio lazima maono yao ya kimaisha yawe sawa na ya wale waliokuwa na akili timamu siku CCM ilipozaliwa.
Vijana wanayo haki ya kufikiria na kuona mambo katika mitazamo tofauti na wakongwe, hivyo CCM wala isione ni dhambi kuongoza nchi huku kwa kasi likiibuka tabaka lenye vionjo tofauti vya kisiasa na kimaisha kwa ujumla.
Ni namna gani vijana hao na wanasiasa hao wanaweza kushawishiwa kwa hoja zinazoambatana na ufanisi wa utekelezaji wa sera zinazobadilika kutokana na wakati, ndio changamoto ya CCM kuelekea miaka 45 mpaka 100 ya uhai wake.
Rangi za chama zinaweza kubaki zile zile, makao makuu yakabaki pale pale, lakini sherehe za miaka 40 ya CCM ziambatane na utayari wa wana-CCM katika kunyumbulika kimtazamo na kimalengo.
Lengo haswa ni kwa chama kuwa na uhalali wa kisiasa, ili mtoto wa leo atakapokuwa ni kijana mwenye mawazo ya kufuatilia siasa basi na akutane na CCM ambayo haitakuwa imeshapitwa na wakati, kwa wakati huo.