Junior Tata
Member
- Oct 18, 2015
- 18
- 2
WanaJF wenzangu nina diploma ya Water Supply Engineering (GPA 4.210), Form 4 nilipata div. II ya point 21 ndo nikachaguliwa technical college, huu n mwaka wa tatu sasa nipo mtaan, naomben msaada
Mkuu ungejiunga na Bachelor degree, ukaendelea na masomo, kwa muda unavoenda, bora ungeendelea na masomo tu!
Pole sana, unaweza kuamua kukusanya wenzako kama 6 hivi wwnye ujuzi kama wako, mkatafuta eneo, kijiji au makazi ya watu. Kisha mkaanzisha mradi wa kusambaza maji katika eneo hilo. Kama upo Dar maeneo ya nje ya mji kama kongowe, mkuranga kuna uhitaji mkubwa wa miradi kama hiyo. Cha kufanya,
1. Anzisheni kampuni na muisajili
2. Fanyeni Tafiti kutafuta eneo ktk kijiji mlichokichagua lenye uwezekano wa kuwa na maji safi yasiyo na chumvi pia na kuangalia watu wangapi wanaweza kuwa wateja wenu
3. Changishaneni mitaji au muangalie uwezekano wa kukopa kama mnakopeshekka.
4. Chimbeni Kisima cha maji na nunueni mashine au mitambo muafaka itakayowezesha kusukuma maji kuwafikia watumiaji.
5. Anzeni kuwaunganisha watumiaji wa maji, kila mteja atanunua vifaa vyake mwenyewe kama mita na mabomba.
Hapo utakuwa umejiajiri tayari.

wazo zur mkuu naweza kukufuata inbox kwa ushaur zaidi?